"

Albamu ya Video

DUWASA Hakikisheni maji hayakatiki Dodoma. Mhe. Aweso

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuhakikisha huduma ya maji inakuwepo muda wote. Amesema Mji wa Dodoma unapokea wageni wengi na hivi karibuni unatarajia kuwapokea wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao watakuwa na kikao kuanzia Julai 11 hadi 12. “Kikubwa tunachowataka sisi kama viongozi wa Wizara ya Maji ni kuhakikisha maji yanapatikana wakati wote, katika kipindi chote kwa wananchi wa Dodoma na wageni wetu wanaokuja katika mkutano huu. Isiwepo sababu yoyote ya mgao usiokuwa wa lazima” amesema Aweso.

Imewekwa: Jul 26, 2020

Urambo, Sikonge, Kaliua, Shelui kunufaika na maji ya ziwa Victoria

Serikali inaendelea na nia yake ya kuhakikisha maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa maji inapatiwa ufumbuzi. Mipango hiyo inahusisha kuupamua mradi wa kusafirisha maji kutoka ziwa Victoria ambao umewezesha maji hayo kufikishwa katika miji ya Tabora, Igunga, Nzega na uyui. Hatua inayofuata sasa ni kuifikia miji na wilaya mbali mbali ikiwemo wilaya ya Urambo, Sikonge na kaliua.

Imewekwa: Jul 26, 2020

Wananchi washirikishwe kuhifadhi vyanzo vya maji. Prof. Nkotagu

Mwenyekiti Bodi ya Maji ya Taifa Professa Hudson Hamisi Nkotagu amewataka wadau wa sekta ya maji nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuwawezesha wananchi kutambua na kushiriki kikamiifu katika zoezi hilo. Amesema wananchi wamezungukwa na fursa nyingi ambazo wanaweza kuzitumia iwapo tu watawezeshwa kuzitambua.

Imewekwa: Jul 26, 2020

Bodi ya Maji Taifa yaridhishwa ushiriki wananchi kutunza vyanzo vya maji.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amewataka wadau wa sekta ya maji nchini kuhakikisha wanawatumia wananchi katika utunzaji vya vyanzo vya maji. agizo hilo amelitoa baada ya kupokea taarifa ya Bodi ya Maji ya Taifa iliyoonesha kuwa chanzo cha maji cha mto Zigi kimeendelea kuboreka kutokana na matumizi ya wananchi kupitia Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira ya Mto Zigi (UWAMAKIZI) taarifa ambayo iliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Hamisi Nkotagu.

Imewekwa: Jul 26, 2020

Bodi ya Maji Taifa yaridhishwa ushiriki wananchi kutunza vyanzo vya maji.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amewataka wadau wa sekta ya maji nchini kuhakikisha wanawatumia wananchi katika utunzaji vya vyanzo vya maji. agizo hilo amelitoa baada ya kupokea taarifa ya Bodi ya Maji ya Taifa iliyoonesha kuwa chanzo cha maji cha mto Zigi kimeendelea kuboreka kutokana na matumizi ya wananchi kupitia Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira ya Mto Zigi (UWAMAKIZI) taarifa ambayo iliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Hudson Hamisi Nkotagu.

Imewekwa: Jun 23, 2020