Sera ya Maji
Sera ya Maji
Maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani, bila maji hakuna uhai. Aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa. Katika hali yake ya asili, maji ni sehemu ya mazingira ambapo wingi na ubora wake ndio unaosaidia katika kuamua jinsi maji yatakavyotumika. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi. Utumiaji wa maji ambayo sio salama na uhaba wa maji huchangia katika kusababisha milipuko na kuenea kwa magonjwa kama kuhara na kipindupindu. Japokuwa maji ni muhimu kwa uhai wa viumbe, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hakuna uwiano wa mgawanyo wa maji ulio sawa kati ya sehemu moja na nyingine na katika majira mbalimbali ya mwaka. Aidha, wingi wa maji yanayofaa kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi una kikomo, na maji hayo pia yanaweza kuathirika kirahisi
Kwa maelezo zaidi bofya hapa