Albamu ya Video
Kumekucha Dodoma. Mashine za kupambana na changamoto ya maji zawasili. Kazi usiku na mchana
Pampu kwa ajili ya visima vya maji vinavyochimbwa eneo la Mzakwe mjini Dodoma zimewasili. Kazi imeanza usiku na mchana ikitarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya huduma ya maji katika jiji hilo
Imewekwa: Jun 03, 2021
Aweso atinga Arumeru na kutoa suluhu ya kukamilika mradi wa maji
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekamilisha ziara ya kikazi mkoani Arusha kwa kukagua ujenzi wa miundombinu ya mradi wa maji katika kijiji cha Ligamba, wilayani Arumeru.
Imewekwa: Jun 03, 2021
Wizara yaja na Luku za maji. zinafanya kazi kama king'amuzi. unajipimia, kama bando la simu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amefanya kikao na kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulika na masuala ya mifugo, maji na kilimo. kikao hicho kilikuwa na lengo la kupata ufahamu wa pamoja wa mifumo ya ukusanyaji wa bili za maji pamoja na mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa mapato, (Unified Billing system). Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mhe. Christine Ishengoma Mhe. Aweso amewahakikishia wajumbe kuwa Wizara ya Maji inaendelea na taratibu mbalimbali zenye lengo la kuondoa changamoto za ulipaji wa bili za maji.
Imewekwa: Jun 03, 2021
#Wikiyamaji. Unapoitwa Mtaalam Tumia taaluma yako kusaidia jamii - Aweso
Unapoitwa Mtaalam Tumia taaluma yako kusaidia jamii - Aweso
Imewekwa: Jun 03, 2021
Haya ndiyo mambo ya Rukwa
Mikakati ya Mkoa wa Rukwa ni kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia kila mwananchi.
Imewekwa: Oct 05, 2020
Bodi za Wakurugenzi za Mamlaka za Maji: "Wajibikeni na fanyeni maamuzi" KM Maji, Mhandisi Sanga
Watendaji wa Mamlaka za Maji wametakiwa kutatua kero za wananchi badala ya kuzizoea na kuziona za kawaida. Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga.
Imewekwa: Oct 05, 2020