Albamu ya Video
Bilioni 40 kumaliza tatizo la maji Musoma
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametembelea mradi wa maji wa Musoma ambao ujenzi wake unaendelea. Mradi huu ambao unatarajia kutumia zaidi ya bilioni 40 utawezesha maeneo mbalimbali ya mji wa musoma kuwa na ziada ya maji safi na salama.
Imewekwa: Aug 24, 2020
Aweso aagiza miradi ya maji Mwanza ikamilike haraka
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa amewataka watalamu wa Wizara kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa katika jiji la Mwanza inakamilishwa haraka.
Imewekwa: Aug 24, 2020
Huduma ya Majisafi yapiga hodi Rombo
Maafisa wa Wizara ya Maji wametembelea mradi wa maji Rombo na kuridhishwa na utekelezaji wake. Mradi huu unalenga kuongeza kiasi cha maji kwenye tanki linalohudumia makao makuu ya wilaya ya Rombo.
Imewekwa: Aug 24, 2020
Zaidi ya wakazi 30,000 kunufaika na mradi wa maji wa Arri-Hasha Wilayani Mbulu
Wakazi wapatao 30,000 wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wa Arri-Hasha unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA) kwa thamani ya shilingi Bilioni 1.6. Mradi huu umefikia asilimia 80 ambapo vituo vya kuchochea maji 14 kati ya 52 vimeanza kutoa huduma
Imewekwa: Aug 24, 2020
Katibu Mkuu Maji ateta na Balozi wa Denmark miradi ya maji Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amekutana na kuzungumza Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji. Mazungumzo hayo ya awali yalilenga ufadhili wa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji hususan kwenye maeneo ya usambazaji wa majisafi na usafi wa mazingira kwenye majiji ya Dodoma na Dar es Salaam, kabla ya kukutana tena na kujadili masuala ya kiufundi katika kutekeleza miradi hiyo
Imewekwa: Aug 17, 2020
Miradi ya Force account imepunguza gharama na muda wa utekelezaji.
Utekelezaji wa miradi ya maji kwa kuwatumia wataalam wa Wizara imesaidia kuokoa muda, na kupunguza gharama. Pia imewezesha miradi hiyo kutekelezwa kwa kutumia vifaa vyenye ubora unaostahili
Imewekwa: Aug 15, 2020