"

Albamu ya Video

Shangwe za mapokezi ya Aweso Kongwa.

Mapema leo WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso alipowasili Kijiji cha Ijaka kata ya Sagara Wilaya ya Kongwa na kupokelewa kwa shangwe na wananchi hasa baada ya kumaliza changamoto yao ya Maji.

Imewekwa: Jun 04, 2021

UNDP wasaidia kulinda vyanzo vya maji Bonde la Mto Wami, Morogoro

Mchango wa UNDP kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji umesaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza jitihada za serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi salama na yenye kutosheleza

Imewekwa: Jun 04, 2021

Waziri Mkuu afungua fursa miundombinu ya maji kutumia bidhaa za viwanda vya ndani

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameagiza vifaa vinavyotumika kutengeneza miundobinu ya maii kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani

Imewekwa: Jun 03, 2021

0:07 / 1:49 Hivi ndivyo Waziri Mkuu alivyokabidhi vitendea kazi kwa Mamlaka za Maji na RUWASA

Mhe. Waziri Mkuu amezindua rasmi Mwongozo wa Usanifu wa Miradi ya Maji (Design Manual) utakaotumika kwenye ujenzi wa miradi yote ya maji nchini, pamoja na kugawa pikipiki 147 zilizotolewa na Serikali kwa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa miradi ya maji kwenye halmashauri zote nchini na magari matatu (3) ya majitaka kwa Mamlaka za Maji.

Imewekwa: Jun 03, 2021

Mapinduzi katika Sekta ya Maji yameleta tabasamu kwa watanzania

Tazama matukio haya yalivyoleta mabadiliko makubwa katika huduma ya maji kwa watanzania

Imewekwa: Jun 03, 2021

Bodi ya Maji ya Taifa yakagua utunzaji rasilimali za maji

Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Maji wametembelea Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe na kujionea utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawi katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya. Programu hiyo inalenga utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kingo za Mto Songwe kwa awamu tatu zinazohusisha upembuzi yakinifu, usanifu na utekelezaji kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili ili kuimarisha mahusiano ya ujirani mwema na kuzingatia misingi ya umoja wa Afrika. Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa, Dkt. Halima Kiwango amesema Wizara ya Maji inafanya kazi nzuri kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa kwa mujibu wa Sheria ya Maji Na. 5 ya Mwaka 2019, akisisitiza kuwa ujenzi wa miradi ya maji ni lazima uende sanjari na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuweza kukidhi mahitaji makubwa ya huduma ya maji kwa wananchi. Akisema kuwa kazi kubwa imefanyika, ila Bodi za Maji za Mabonde ziongeze jitihada zaidi na kumaliza changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji na kuliondoloea taifa hatari ya kuingia kwenye hali ya uhaba wa maji. Aidha, wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa wametembelea na kujionea shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji zinazofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa kwa kukagua chanzo cha maji cha Nyibuko pamoja na kituo cha kupima wingi na usawa wa maji kwenye mto Kiwira katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya na kuridhishwa na maendeleo yake. Wajumbe hao wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika na kusababisha wingi na ubora wa maji kwenye chanzo cha maji cha Nyibuko ambacho chemchemi yake inapeleka maji yake kwenye mto Nyibuko kuongezeka, ambao unamwaga maji yake kwenye mto Kiwira.

Imewekwa: Jun 03, 2021