"

Albamu ya Video

Bili bambikizi za Maji zifike Mwisho- Mhe. Aweso.

Waziri Aweso ametumia wasaa wa ziara yake Mkoani Mwanza kwenye Mradi wa Maji Buswelo kuwaelekeza Meneja Masoko (Commercial Manager) wote wa Mamlaka za Majisafi kusimamia kikamilifu zoezi la usomaji mita za maji ziwe halisia ili kuepuka kuwabambikia wananchi bill za maji. Mh. Aweso amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji kuwasimamia Meneja Masoko wa Mamlaka za Maji wasiwape wasoma mita za maji malengo makubwa ya makusanyo (target) yasiyo halisia ambayo hayatekelezeki na yanawaumiza wananchi na kusababisha malalamiko akisisitiza kero hii ifike mwisho.

Imewekwa: Jun 04, 2021

Wizara za Maji Zanzibar na Tanzania Bara waahidi kudumisha ushirikiano

Wizara za Maji Zanzibar na Tanzania Bara waahidi kudumisha ushirikiano

Imewekwa: Jun 04, 2021

Aweso awataka Watumishi wa Wizara kuzingatia Sheria.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka watumishi wa Wizara ya Maji kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija katika utendaji kazi. Wito huo ameutoa leo Mei 3, 2021 mjini Dodoma wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo. Amesema Vyama na Mabaraza ya wafanyakazi yameundwa kwa sababu za msingi za kuhakikisha kunakuwepo na ufanisi katika utendaji kazi. Bila kufanya hivyo Vyama au Mabaraza ya wafanyakazi yatakuwa yanachochea migogro na malalamiko katika sehemu ya kazi. “Mahali ambapo Chama au Baraza la Wafanyakazi, kazi yake kubwa ni kushughulikia tu kero za watumishi bila kusimamia viwango vya uzalishaji au ufanisi wa kazi, pataendelea kuwa na migogooro isiyoisha ya watumishi wanaodai maslahi bila kutimiza wajibu.” Aweso amesema. Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji itahakikisha inatoa ushirikiano kwa Vyama na Mabaraza ya Wafanyakazi kwani kufanya hivyo kunasaidia kuwa karibu na wadau wa sekta ya Maji na hivyo kurahisisha suala zima la upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wananchi.

Imewekwa: Jun 04, 2021

Kamati ya Maji ya Bunge yaridhishwa na kasi ya utekelezaji miradi ya maji Dodoma

kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea maeneo mbalimbali katika jiji la Dodoma na kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) kuondoa changamoto ya upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wakazi wa jiji la Dodoma. Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Christine Ishengoma (Mb) amesema kamati imeridhishwa na jitihada zinazofanywa na serikali na kwamba matumaini ya kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji Katika jiji ziko wazi ndani ya muda mfupi. Amesema Kamati inatambua kipindi kigumu wanachopitia wananchi wa jiji la Dodoma Katika kupata huduma ya majisafi lakini wasife moyo matumaini yapo na yanaonekana wazi. “Niwapongeze viongozi wa Wizara ya Maji kwa jinsi mnavyohangaika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji. Sisi sote tunatambua kwamba baada ya Serikali kuhamia Dodoma, idadi ya watu iliongezeka na kusababisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama, lakini kwa jinsi mnavyokwenda ni wazi tatizo hili linaweza kuisha hata ndani ya mwaka mmoja”. Amesema Dkt. Ishengoma. Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema wanafanya kila jitihada kuhakikisha mji wa Dodoma unapata Maji na hivyo kuondoa kabisa changamoto hiyo. Niwahakikishie kuwa sisi Viongozi wa Wizara ya maji hatutakuwa kikwazo kuhakikisha wananchi wa Dodoma wanapata majisafi, salama na yenye kutosheleza. Kamati hiyo imetembelea maeno ya Mzakwe kwenye vyanzo vya maji yanayohudumia mji wa Dodoma pamoja na eneo la Chamwino kunakojengwa tenki kubwa lenye uwezo wa kuzalsiha lita milioni mbili na laki tano.

Imewekwa: Jun 04, 2021

Dkt. Bashiru Ally atoa ushauri kuhusu miradi ya maji. Ni baada ya kufanya ukaguzi jijini Dodoma

Balozi Dkt Bashiru Ally (Mb) ameshauri Wizara ya Maji kuwa na utaratibu utakaowezesha kuendelea kuzalisha wataalam wa masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya maji. Ushauri huo ameutoa Leo Mei, 4, 2021 wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kukagua utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dodoma

Imewekwa: Jun 04, 2021

#MAJINIUHAI IRUWASA inavyoboresha huduma ya maji IringaTazama mafanikio

Tazama mafanikio katika uboreshaji wa huduma ya maji Iringa

Imewekwa: Jun 04, 2021