Albamu ya Video
Sasa mteja wa maji kupata huduma ndani ya sku Saba
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ameziagiza Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kote nchini kuhakikisha wananawaunganishia wateja wapya ndani ya siku saba.
Imewekwa: Aug 10, 2020
Majisafi na Salama. Sasa ni zamu ya Mbalizi
Wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya wameanza kupata huduma ya majisafi na salama kufuatia utekelezaji wa mradi wa maji wa Mbalizi ambao umetekelezwa na Mamlaka ya majisafi na USafi wa Mazingira Mbeya. Mradi huo ni moja ya añadí alizozitoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Imewekwa: Aug 10, 2020
Mbunge Kitwanga afurahishwa na kasi ya usambazaji maji nchini
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Misungwi Mkoani Mwanza (2015-2020) Mhe. Charles Kitwanga amefurahishwa na kasi ya usambazji maji nchini. Amesema amekuwa akitembelea Mamka za Maji ikiwemo ile inayosimamia usambazaji maji yanayotokea ziwa Victoria kwenda Mikoa ya Mwanza, Geita, Tabora na Shinyanga (KASHWASA) na kuridhishwa na Utendaji kazi wao.
Imewekwa: Jul 26, 2020
DUWASA Hakikisheni maji hayakatiki Dodoma. Mhe. Aweso
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuhakikisha huduma ya maji inakuwepo muda wote. Amesema Mji wa Dodoma unapokea wageni wengi na hivi karibuni unatarajia kuwapokea wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao watakuwa na kikao kuanzia Julai 11 hadi 12. “Kikubwa tunachowataka sisi kama viongozi wa Wizara ya Maji ni kuhakikisha maji yanapatikana wakati wote, katika kipindi chote kwa wananchi wa Dodoma na wageni wetu wanaokuja katika mkutano huu. Isiwepo sababu yoyote ya mgao usiokuwa wa lazima” amesema Aweso.
Imewekwa: Jul 26, 2020
Urambo, Sikonge, Kaliua, Shelui kunufaika na maji ya ziwa Victoria
Serikali inaendelea na nia yake ya kuhakikisha maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa maji inapatiwa ufumbuzi. Mipango hiyo inahusisha kuupamua mradi wa kusafirisha maji kutoka ziwa Victoria ambao umewezesha maji hayo kufikishwa katika miji ya Tabora, Igunga, Nzega na uyui. Hatua inayofuata sasa ni kuifikia miji na wilaya mbali mbali ikiwemo wilaya ya Urambo, Sikonge na kaliua.
Imewekwa: Jul 26, 2020
Wananchi washirikishwe kuhifadhi vyanzo vya maji. Prof. Nkotagu
Mwenyekiti Bodi ya Maji ya Taifa Professa Hudson Hamisi Nkotagu amewataka wadau wa sekta ya maji nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuwawezesha wananchi kutambua na kushiriki kikamiifu katika zoezi hilo. Amesema wananchi wamezungukwa na fursa nyingi ambazo wanaweza kuzitumia iwapo tu watawezeshwa kuzitambua.
Imewekwa: Jul 26, 2020