Albamu ya Video
Kamati ya Maji ya Bunge yaridhishwa na kasi ya utekelezaji miradi ya maji Dodoma
kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea maeneo mbalimbali katika jiji la Dodoma na kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) kuondoa changamoto ya upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wakazi wa jiji la Dodoma. Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Christine Ishengoma (Mb) amesema kamati imeridhishwa na jitihada zinazofanywa na serikali na kwamba matumaini ya kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji Katika jiji ziko wazi ndani ya muda mfupi. Amesema Kamati inatambua kipindi kigumu wanachopitia wananchi wa jiji la Dodoma Katika kupata huduma ya majisafi lakini wasife moyo matumaini yapo na yanaonekana wazi. “Niwapongeze viongozi wa Wizara ya Maji kwa jinsi mnavyohangaika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji. Sisi sote tunatambua kwamba baada ya Serikali kuhamia Dodoma, idadi ya watu iliongezeka na kusababisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama, lakini kwa jinsi mnavyokwenda ni wazi tatizo hili linaweza kuisha hata ndani ya mwaka mmoja”. Amesema Dkt. Ishengoma. Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema wanafanya kila jitihada kuhakikisha mji wa Dodoma unapata Maji na hivyo kuondoa kabisa changamoto hiyo. Niwahakikishie kuwa sisi Viongozi wa Wizara ya maji hatutakuwa kikwazo kuhakikisha wananchi wa Dodoma wanapata majisafi, salama na yenye kutosheleza. Kamati hiyo imetembelea maeno ya Mzakwe kwenye vyanzo vya maji yanayohudumia mji wa Dodoma pamoja na eneo la Chamwino kunakojengwa tenki kubwa lenye uwezo wa kuzalsiha lita milioni mbili na laki tano.
Imewekwa: Jun 04, 2021
Dkt. Bashiru Ally atoa ushauri kuhusu miradi ya maji. Ni baada ya kufanya ukaguzi jijini Dodoma
Balozi Dkt Bashiru Ally (Mb) ameshauri Wizara ya Maji kuwa na utaratibu utakaowezesha kuendelea kuzalisha wataalam wa masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya maji. Ushauri huo ameutoa Leo Mei, 4, 2021 wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kukagua utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dodoma
Imewekwa: Jun 04, 2021
#MAJINIUHAI IRUWASA inavyoboresha huduma ya maji IringaTazama mafanikio
Tazama mafanikio katika uboreshaji wa huduma ya maji Iringa
Imewekwa: Jun 04, 2021
Shangwe za mapokezi ya Aweso Kongwa.
Mapema leo WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso alipowasili Kijiji cha Ijaka kata ya Sagara Wilaya ya Kongwa na kupokelewa kwa shangwe na wananchi hasa baada ya kumaliza changamoto yao ya Maji.
Imewekwa: Jun 04, 2021
UNDP wasaidia kulinda vyanzo vya maji Bonde la Mto Wami, Morogoro
Mchango wa UNDP kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji umesaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza jitihada za serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi salama na yenye kutosheleza
Imewekwa: Jun 04, 2021
Waziri Mkuu afungua fursa miundombinu ya maji kutumia bidhaa za viwanda vya ndani
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameagiza vifaa vinavyotumika kutengeneza miundobinu ya maii kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani
Imewekwa: Jun 03, 2021