Albamu ya Video
0:07 / 1:49 Hivi ndivyo Waziri Mkuu alivyokabidhi vitendea kazi kwa Mamlaka za Maji na RUWASA
Mhe. Waziri Mkuu amezindua rasmi Mwongozo wa Usanifu wa Miradi ya Maji (Design Manual) utakaotumika kwenye ujenzi wa miradi yote ya maji nchini, pamoja na kugawa pikipiki 147 zilizotolewa na Serikali kwa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa miradi ya maji kwenye halmashauri zote nchini na magari matatu (3) ya majitaka kwa Mamlaka za Maji.
Imewekwa: Jun 03, 2021
Mapinduzi katika Sekta ya Maji yameleta tabasamu kwa watanzania
Tazama matukio haya yalivyoleta mabadiliko makubwa katika huduma ya maji kwa watanzania
Imewekwa: Jun 03, 2021
Bodi ya Maji ya Taifa yakagua utunzaji rasilimali za maji
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Maji wametembelea Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe na kujionea utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawi katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya. Programu hiyo inalenga utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kingo za Mto Songwe kwa awamu tatu zinazohusisha upembuzi yakinifu, usanifu na utekelezaji kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili ili kuimarisha mahusiano ya ujirani mwema na kuzingatia misingi ya umoja wa Afrika. Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa, Dkt. Halima Kiwango amesema Wizara ya Maji inafanya kazi nzuri kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa kwa mujibu wa Sheria ya Maji Na. 5 ya Mwaka 2019, akisisitiza kuwa ujenzi wa miradi ya maji ni lazima uende sanjari na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuweza kukidhi mahitaji makubwa ya huduma ya maji kwa wananchi. Akisema kuwa kazi kubwa imefanyika, ila Bodi za Maji za Mabonde ziongeze jitihada zaidi na kumaliza changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji na kuliondoloea taifa hatari ya kuingia kwenye hali ya uhaba wa maji. Aidha, wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa wametembelea na kujionea shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji zinazofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa kwa kukagua chanzo cha maji cha Nyibuko pamoja na kituo cha kupima wingi na usawa wa maji kwenye mto Kiwira katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya na kuridhishwa na maendeleo yake. Wajumbe hao wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika na kusababisha wingi na ubora wa maji kwenye chanzo cha maji cha Nyibuko ambacho chemchemi yake inapeleka maji yake kwenye mto Nyibuko kuongezeka, ambao unamwaga maji yake kwenye mto Kiwira.
Imewekwa: Jun 03, 2021
Aweso akemea ubadhirifu Jumuia za watumia maji
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amekemea ubadhilifu unaofanywa na jumuia za watumia maji na kuagiza miradi isimamiwe na watalaam.
Imewekwa: Jun 03, 2021
#MAJINIUHAI TEHAMA ilivyoboresha huduma sekta ya maji
TEHAMA Katika sekta ya maji
Imewekwa: Jun 03, 2021
Maboresho katika huduma ya maji yamepunguza magonjwa ya mlipuko- Wataalam wa Maji
Maboresho katika huduma ya maji yamepunguza magonjwa ya mlipuko- Wataalam wa Maji
Imewekwa: Jun 03, 2021