Habari

Imewekwa: Nov, 18 2026

​Ahadi ya bilioni 4 mwisho wa mwezi Novemba, yatekekezwa ndani ya siku mbili.

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemwambia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi kuwa bilioni 4 zilizoahidiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Novemba 2026 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa maji Makonde mkoani Mtwara Rais Samia ameruhusu na tayari fedha zimefikishwa kwa mkandarasi ndani ya siku mbili.

Ahadi hiyo ilitolewa Novemba 12, 2026 kufuatia maombi ya wabunge wa majimbo ya Wilaya za Tandahimba, Newala na Mtwara wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mkoani hapo.

Mhe. Aweso ameyasema hayo Katika ziara ya Makamu wa Rais Katika eneo la Madangwa wilayani Lindi.

Amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza utekekezaji wa haraka wa utoaji wa fedha za Miradi hivyo wananchi wa Madangwa na maeneo yote yenye Miradi ya Maji wasiwe na mashaka.

Aidha, Mhe. Aweso amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nauye kuleta miilioni 500 ndani ya siku mbili kwa ajili ya utekelezaji mradi wa Maji utakaohudumia wananchi eneo la Madangwa wilayani Lindi.

Amesema utekekezaji wa mradi utafanyika bila kuchelewa, huduma ya majisafi na salama itaanza kupatikana kwa wananchi wa Madangwa ndani ya miezi miwili.