Vitengo

Kitengo cha Kuandaa Miradi, Uratibu na Usimamizi wa Mazingira

Lengo

Kuandaa miradi na kuratibu ushirikiano baina ya wizara na washirika wa maendeleo na wadau wengine katika sekta ya maji.

Kazi zifuatazo zinatekelezwa na kitengo:-

(i) Kuandaa viwango vya usanifu na menejimenti ya miradi ya maji

(ii) Kutoa ushauri wa kitaalam kwa Taasisi na Wakala kuhusu usanifu wa miradi ya maji

(iii) Kufanya mapitio na kushauri kuhusu usanifu wa miradi

(iv) Kutunza kanzidata ya miradi ya maji (iliyokamilika, inayoendelea na inayotarajia kutekelezwa)

(v) Kuratibu ufunguzi wa miradi ya maji iliyokamilika kwa kushirikiana na Idara na Taasisi

(vi) Kuratibu mahitaji ya rasilimali za utekelezaji wa miradi ya maji kwa kushirikiana na Idara ya Sera na Mipango pamoja na Idara nyingine za utekelezaji

(vii) Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji kwa kuhakikisha uzingiatiaji wa viwango vya ujenzi vya nchi na kimataifa, utekelezaji wa mradi kwa wakati na thamani ya fedha, na kuzingatia masuala ya mazingira na jamii;

(viii) Kujenga uwezo wa watumishi/wataalam katika usimamizi na ujenzi wa miradi ili kupata thamani halisi ya fedha;

(ix) Kuwa kiungo kati ya wizara na washirika wa maendeleo na wadau wengine

(x) Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika kuendeleza sekta ya maji.

Kitengo kinaongozwa na Mkurugenzi

Kitengo cha Fedha na Uhasibu

Lengo

Kufanya kazi ya menejimenti na utunzaji wa fedha.

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

Mshahara

(i) kuandaa na kufanya malipo ya mshahara kwa wakati ;

(ii) Menejimenti ya orodha ya malipo; na

(iii) Bajeti ya stahili

Ofisi ya Fedha

(i) Kuratibu masuala yote yanayohusu malipo.

Mapato

(i) Makusanyo ya mapato; na

(ii) Kuratibu ukusanyaji wa mapato.

Pensheni

(i) Kuandaa nyaraka za malipo kwa wakatition ; na

(ii) Kutunza kumbukumbu kuhusu pensheni.

Bajeti

(i) Kuandaa bajeti; na

(ii) Kufuatilia matumizi.

Ukaguzi

(i) Kupitia na kuhakikisha nyaraka za malipo zina viambatisho vinavyostahili kuendana na taratibu zilizopo;

(ii) Kupitia nyaraka za kifedha kama zimezingatia Sheria, Kanunia, Taratibu na Miongozo iliyopo; na

(iii) Kutoa mrejesho kuhusu hoja za kikaguzi.

Kitengo kinaongozwa na Mhasibu Mkuu.

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Lengo

Kushauri na kuratibu matumizi bora ya rasilimali.

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kukagua taarifa na rikodi za kifedha;

(ii) Kukagua taarifa ili kuhakikisha zimeandaliwa kwa kuzingatia taratibu na sheria za matumizi;

(iii) Kukagua na kupitia taarifa za akaunti za mapato na matumizi kuhakikisha taratibu zimezingatiwa;

(iv) Kuandaa taratibu za ukaguzi kwa mujibu wa viwango vya kimataifa;

(v) kukagua, kupitia na kuandaa ripoti za kifedha na ripoti nyingine;

(vi) Kupitia na kuandaa ripoti kuhusu mifumo ya utunzaji rasilimali na uhakiki wake;

(vii) Kupitia na kutoa ripoti kuhusu matokeo ya kazi / programu kama yanaendana na lengo/ malengo yalivyopangwa;

(viii) Kushauri na kusaidia katika utekelezaji wa maelekezo ya ripoti mbalimbali za kikaguzi;

(ix) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu uthibiti na utoshelevu wa mifumo ya TEHAMA;

(x) Kuandaa na kutekeleza mkakati wa ukaguzi ; na

(xi) Kufanya ukaguzi wa utendaji katika miradi ya maendeleo.

Kitengo kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani.

Kitengo cha Manunuzi

Lengo

Kutoa usaidizi na utaalam katika manunuzi ya vitu na huduma, utunzaji na usambazaji wa vifaa.

kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kushauri masuala yanayohusu manunuzi ya vitu na huduma,pamoja na menejimenti yake;

(ii) Kusimamia na kuhakikisha taratibu za manunuzi zinafuatwa kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi;

(iii) Kuandaa mpango wa manunuzi kila mwaka;

(iv) Kununua, kutunza na kusimamia usambazaji wa vitu na huduma mbalimbali ;

(v) Kutunza daftari la manunuzi;

(vi) Kushiriki kama katibu wa Kamati ya Manunuzi ya Wizara kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi;

(vii) Kuweka viwango vya vitu na huduma zinazo nunuliwa na kufuatilia vina ubora wa thamani ya fedha ; na

(viii) Kuandaa bajeti na ripoti mbalimbali za Kitengo.

Kitengo kitaongozwa na Mkurugenzi.

Kitengo cha Huduma za Sheria

Lengo

Kutoa ushauri wa kisheria kwa wizara

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kutoa ushauri kwa wizara na taasisi zake katika masuala yote ya kisheria;

(ii) Kushiriki katika kuandaa na kutoa usaidizi katika kuandaa masuala ya machapisho ya kisheria, na sheria kabla ya kuwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu;

(iii) Kufuatilia na kujibu masuala ya kisheria Mahakamani na kutunza kumbukumbu za maamuzi ya Mahakama.

Kitengo kinaongozwa na Mkurugenzi.

Kitengo cha TEHAMA

Lengo

Kutoa ushauri na utaalam kuhusu masuala ya TEHAMA .

Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kutekelezaji wa sera ya TEHAMA na Serikali mtandao;

(ii) Kuunda na kuratibu mfumo shirikishi wa TEHAMA wa wizara;

(iii) Kutunza na kuhakikisha mifumo ya TEHAMA na vifaa vyake iko salama;

(iv) Kuratibu na kusaidia utaalamu katika ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA;

(v) Kuanzisha na kuratibu matumizi ya barua pepe (za ndani na nje ya wizara); na

(vi) Kufanya utafiti na kushauri maeneo yanayoweza kutumia TEHAMA kama nyenzo ya kuongeza ubora katika utoaji huduma.

Kitengo kinaongozwa na Mtehama Mkuu.

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Lengo

Kuratibu mawasiliano kati ya wizara na wadau wake

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kuandaa machapisho ya elimu kwa umma kuhusu sera, programu na kazi mbalimbali zinazotekelezwa na wizara;

(ii) Kuratibu vyombo vya habari katika kazi za wizara;

(iii) Kuwashirikisha wananchi kwa kutoa taarifa pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara;

(iv) Kutangaza kazi za wizara ;

(v) Kuratibu machapisho na mada kwa ajili ya mikutano na makongamano;

(vi) Kuratibu na kuandaa makala mbalimbali kuhusu wizara; na

(vii) Kuweka taarifa kila wakati katika tovuti ya wizara na mitandao ya kijamii.

Kitengo kinaongozwa na Afisa Habari Mkuu.