Habari

Imewekwa: Feb, 27 2024

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amezindua mradi wa maji wa Misisi Zanzibar

News Images

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amezindua mradi wa maji wa Misisi Zanzibar na kusisitiza mradi huo utoe huduma saa 24.

Amesema utaratibu wa kupeleka maji vijijini ni wa tangu Rais Samia akiwa Makamu wa Rais alipoanzisha kampeni ya "kumtua mama ndoo kichwani" na kuhakikisha maji yanafika kila sehemu.

Amesema mradi wa maji wa Misisi Zanzibar katika kata ya Sazira, mji wa Bunda utaendelea kuongezewa maji kutoka ziwa victoria

Mhe. Majaliwa amewasisitiza wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali kwani inaendelea na mikakati ya kutatua changamoto ya maji katika maeneo yote ambayo yanatakiwa kufikiwa na huduma hiyo .

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa miaka ya nyuma viongozi wengi waliofika katika mji wa Bunda walikuwa wakipokelewa na ndoo za maji, kutokana na changamoto ya kutokamilika kwa miradi ya maji na fedha zilizokuwa zikitolewa.

Amesema kuwa wananchi wa Bunda wanahitaji lita milioni 9,na mradi wa Chujio wa Nyabehu unauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 15 na Wizara ya Maji ipo tayari kuhakikisha kila eneo wanapata huduma ya maji safi.

Amesema ni haki ya kila mwananchi kupata huduma ya maji na apate bili kutokana na matumizi yake ambapo wizara inatarajia kutumia mfumo wa luku kwa ajili ya malipo ya maji .

Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWASSA), Bi. Esther Gilyoma kwa kazi nzuri pamoja na kukamilika kwa mradi mkubwa wa kusambaza maji wa Nyabehu.

Taarifa ya mradi iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji mjini Bunda Bi.Esther Gilyoma inaonesha kuwa mradi wa Misisi Zanzibar umetekelezwa na wataalam wa ndani (force account) na kugharimu shilingi milioni 700.

Kitengo cha Mawasiliano