Habari

Imewekwa: Sep, 22 2025

​Waziri Aweso awapa heko timu Maji kwa ushindi wa Michezo SHIMIWI

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameipongeza timu ya michezo ya Wizara ya Maji (Maji Sport) kwa ushindi walioupata katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Jijini Mwanza.

Pongezi hizo amezitoa kwa njia ya simu kutokea Pangani mkoa wa Tanga baada ya timu hiyo kufika ofisini kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji kumkabidhi vikombe vinne vya ushindi vilivyopatikana katika mashindano hayo.

Vikombe hivyo ni kikombe cha mshindi wa kwanza mchezo wa mishale (Darts) na Mchezo wa Draft, wote wanaume. Mshindi wa kwanza Karata na mshindi wa pili Bao kwa timu ya wanawake.

Amesema ushindi huo ni heshima kwa Wizara ya Maji na uthibitisho kuwa kila jambo linaloihusu Wizara ya Maji linazingatiwa kama shughuli maalumu na kupewa kipaumbele cha maandalizi.

Aidha, ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa ushindi huo.

Naye katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Mwajuma Waziri amesema yeye binafsi amefurahishwa na ushindi huo.

Amesema mwisho wa mchezo huo ni maandalizi kwa michezo mingine kwa mwaka 2026