Habari

Imewekwa: Apr, 16 2026

​WAZIRI AWESO ATOA AGIZO KALI KUDHIBITI MAJI YASIYOLIPIWA

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb.) amezitaka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kuhakikisha wanadhibiti maji yasiyolipiwa (NRW) katika maeneo wanayotoa huduma.

Amesema tathmini iliyofanywa na Wizara ya Maji imebaini yapo baadhi ya maeneo yapo vizuri na baadhi ya maeneo yana changamoto ya upotevu wa maji.

Ameyasema hayo wakati akizindua bodi ya 10 ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na kusisitiza moja ya kipimo cha utendaji kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji ni suala la kusimamia udhibiti wa upotevu wa maji.

“Niwaombe na niwasihi sana watendaji wa Mamlaka zetu za maji twendeni tukadhibiti upotevu wa maji, faraja ya Mkurugenzi wa maji ni wananchi kupata maji,” Mhe. Aweso amesema.

Ameongeza kuwa jambo ambalo halimfurahishi ni upotevu wa maji, akisisitiza kuwa faraja yake kubwa ni huduma hiyo kuwafikia wananchi na sio kupotea.

Waziri Aweso ameomba ushirikishwaji wa viongozi wa mikoa na wilaya kupitia kamati za ulinzi na usalama katika wa miundombinu ya maji wanashitakiwa kwa taratibu zilizopo.

Kitengo cha Mawasiliano