Habari

Imewekwa: May, 20 2026

Wadau wakaribishwa kuwekeza uhifadhi ziwa Victoria

News Images

Wadau wa Sekta ya Maji wamekaribishwa kuwekeza katika uhifadhi wa ziwa Victoria.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Bi. Rose Ambrose amewaalika wadau wa maendeleo kuwekeza katika uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za maji za Ziwa Victoria.

Amesema hayo akifungua warsha ya wadau wa Bonde la Ziwa Victoria katika maadhimisho ya kwanza ya ziwa victoria jijini Mwanza.

Amesema kazi ya uhifadhi na uendelezaji wa ziwa Victoria inahitaji fedha, utangamano na ushirikiano katika ngazi zote kwasababu changamoto za maji Duniani kama vile upungufu wa maji, ukame, mafuriko, uchafuzi na athari za mabadiliko ya tabianchi ni kubwa na zimeshavuka mipaka ya kiutawala.

“Maji yanalazimisha jamii kuungana na kushirikiana.” Amehitimisha kwa kualika nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jamuiya ya Kimataifa, Washirika wa Maendeleo, Wana Taaluma na Watafiti, Asasi za Karaia, na wadau wengine kushiriki katika kuhifadhi na kulinda Ziwa hilo.

“Kila mmoja akiwa balozi mzuri wa uhifadhi wa ziwa Victoria kwa maana ya kufanya shughuli za uhifadhi na kuzuia shughuli hatarishi, tutafanikiwa.”

Warsha imehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi ikiwa na kaulimbiu ‘Maji Yetu, Mustakabali Wetu: Tuungane kwa Usimamizi Endelevu wa Bonde la Ziwa Victoria’ .