Habari

Imewekwa: Oct, 31 2023

​Visima 450 kuchimbwa Kibiti & Simanjiro

News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu amesaini mkataba wa makubaliano na Asasi ya Mtandao wa Msaada (Global Aid Network) ya Canada kuhusu kazi ya uchimbaji wa visima vya maji vipatavyo 450.

Hafla ya utiaji Saini imefanyika Jijini Dodoma na Asasi hiyo imewasilishwa na Meneja Uendeshaji na Ufundi Bw. Stephen Thomson

Visima hivyo vitachimbwa Kibiti na Simanjiro, na kila mwaka vitachimbwa visima 90 kwa kipindi cha miaka mitano ya mkataba. Urefu na kiwango cha uchimbaji kwenda chini itakuwa mita 200.

Kitengo cha Mawasiliano