Habari

Imewekwa: Jan, 28 2021

Uzinduzi Miradi ya Maji Shinyanga na Tabora

News Images

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi miwili mikubwa ya Maji kutoka Ziwa Victoria.

Mradi wa kwanza unapeleka maji katika miji midogo ya Kagongwa na Isaka Mkoani Shinyanga na mradi wa pili unapeleka maji katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega Mkoani Tabora.

Mradi wa Kagongwa-Isaka umetekelezwa kwa fedha za ndani kiasi cha Shilingi Bilioni 23.1 na utazinduliwa siku ya Ijumaa Januari 29, 2021 katika uwanja wa Isagehe uliopo kata ya Isagehe wilayani Kahama, na ule wa Tabora -Igunga - Nzega ambao umetekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 617 utazinduliwa siku ya Jumamosi Januari 30, 2021 Mjini Tabora katika eneo la Kaze Hill.

Miradi yote miwili inatarajiwa kumaliza tatizo la maji kwa wananchi zaidi ya milioni 1.3.

Wananchi wa maeneo husika pamoja na wananchi wote mnakaribishwa kushuhudia mafanikio haya makubwa na ya kihistoria kwa nchi yetu.