Habari

Imewekwa: Mar, 16 2022

Uteuzi

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Orkesumet-Simanjiro, iliyopo wilayani Simanjiro.

Waziri Aweso amefanya uteuzi huu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Maji 2022, ambapo mradi mkubwa wa maji wa Orkesumet wenye thamani ya shilingi bilioni 41.5 umewekewa jiwe la msingi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Isidor Mpango.

Aliyeteuliwa ni Mhandisi Amedeus Kisaka ambaye ametumikia nafasi ya Meneja Ufundi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Babati. Mhandisi Kisaka anao uzoefu mkubwa katika Sekta ya Maji, hususani eneo la usimamizi wa miradi ya maji.

Uteuzi huu unaanza mara moja, kuanzia tarehe 15 Machi, 2022

Kitengo cha Mawasiliano