Habari

Imewekwa: Feb, 13 2024

Tutafute fedha zaidi katika maji- Mhandisi Mwajuma

News Images

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wadau wa Sekta Mtambuka kuongeza nguvu zaidi katika kupata fedha na kushirikiana na Serikali katika kufanikisha masuala anuai yahusuyo huduma ya maji kwa Watanzania.


Amesema hayo akifunga Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji Jijini Dar es Salaam.


Amesisitiza umuhimu wa kuongeza wadau wa Jukwaa ili kuyafikia makundi mengi katika jamii pia kuongeza nguvu ya ushirikishwaji.


Amesema ni muhimu kuwa na mipango inayotekelezeka ya kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubalika na jamii.


Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam likiwa limebeba kaulimbiu isemayo; Majanga ya Mafuriko na Ukame: Uwekezaji katika Usalama wa Maji ni Jambo la Haraka.


Mhandisi Mwajuma ni mmoja kati ya vinara wanawake katika masuala ya uhandisi na huduma kwa jamii hapa nchini.