Habari

Imewekwa: May, 03 2026

Wananchi Waishukuru Serikali kwa Kuhamasisha Uoteshaji wa Miti Kwenye Vyanzo

News Images

Wananchi wa Kijiji cha Dudiye Wilayani Babati Mkoa wa Manyara wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwamo chanzo cha maji cha Mtoto Bubu mkoani humo.

Wakizungumza katika Shule ya Msingi Dudiye palipofanyika zoezi la uoteshaji miti wameeleza maeneo ya vijijini bado uelewa ni mdogo kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji.

Wameshauri Serikali kuweka mpango maalumu wa mara kwa mara Ili kuendelea kutoa elimu.

Zoezi hilo la uoteshaji wa miti limeongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, anayesimamia uhifadhi wa vyanzo vya maji Bi. Rosemary Rwebugisa akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara wa Maji.

Zoezi hilo ni muendelezo wa jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji katika Programu ya Uhimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa lengo la kuhifadhi chanzo hicho kwa ajili ya uendelevu wa Bwawa la Farkwa llinalotarajiwa kujengwa wilayani Chemba, mkoani Dodoma.