Habari

Imewekwa: Aug, 13 2023

Mradi wa maji wa milioni 798.7 wazinduliwa Mtwara

News Images

Mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 798.7 umezinduliwa Tandahimba, mkoani Mtwara na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim MajaliwaMajaliwa (Mb).

Mhe.Majaliwa ameipongeza Wizara ya Maji kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji nchini na kusisitiza kuwa wananchi walinde miundombinu ya miradi ya maji pamoja na kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ili miradiinayotekelezwa iwe endelevu.

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) katika uzinduzi huo amesema mradi huo wa majisafi wa Kitama,pamoja na mengine umehusisha, ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 20.1 , na ujenzi wa vizimba vya umma vya kuchotea maji 10.

Ameongeza Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika miji 28 ambapo kwa Wilaya ya Tandahimba mkandarasi ameshaanza utekelezaji wa mradi wa maji wa Makonde kwa gharama ya shilingi bilioni 84 na ameshalipwa shilingi bilioni 12 za kuanza utekelezaji.

Kitengo cha Mawasiliano