Habari

Imewekwa: Nov, 11 2023

​Maji na TCM waandaa mafunzo kuhusu mabwawa ya Tope Sumu

News Images

Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) imeandaa mafunzo ya siku tatu kuhusu Usalama wa Mabwawa ya Tope Sumu (TSF) na Mabwawa ya maji ya kawaida kwa usalama wa mazingira na wananchi.

Mafunzo hayo yatafanyika amefanyika mkoani Mwanza kuanzia tarehe 28-30 Novemba,2023.

Taarifa kwa vyombo vya habari ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu iliyosomwa naMhandisi Mkuu wa Mabwawa Edward Robertimesemausalama wa mabwawa ya Tope Sumu katikamigodi ni muhimu kuthibiti yasilete madhara kwa jamii kwa kuhakikisha ujenzi wake, ukarabati na njia za udhibiti wa madhara zinafuata Sheria,Kanuni, Taratibu, Miongozo na taratibu mahsusi za ujenzi wa mabwawa.

Mwenyekiti wa Chemba ya Madini Tanzania, Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema malengo ya kuandaliwa kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu na wasimamizi wa mabwawa ya Tope sumu katika migodi ili kuwa na njia thabiti na tahadhari za kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na mabwawa hayokwa Jamii.

Kitengo cha Mawasiliano