Habari

Imewekwa: May, 26 2023

Sekta ya Maji tushirikiane na sekta binafsi

News Images

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka viongozi wa Sekta ya Maji kushirikiana na sekta binafsi katika kutatua changamoto pale zinapoibuka katika Sekta ya Maji. Ameyasema hayo wakati akifunga Kikao cha Majadiliano kati ya Wizara ya Maji na wadau wa Maendeleo (Thematic Working Group) kilichohusu rasilimali za maji na ubora wa maji hapa nchini.

Kikao kazi hicho kimefanyika jijijini Dodoma, kikishirikisha wajumbe wengine kutoka maeneno mbalimbali Duniani kwa njia ya mtandao wa Intaneti.

Amesema Wizara ya Maji haiwezi kujitenga na sekta binafsi katika masuala yote yanayoihusu Sekta ya Maji kwa sababu sekta zote zinalenga kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.

Amewashukuru wadau wote na kuwahakikishia kuwa serikali iko pamoja nao kwani inatambua wazi kuwa bila ushirikishwaji wa wadau, Serikali peke yake haiwezi kufikia malengo.