Habari

Imewekwa: Sep, 13 2025

Katibu Mkuu Maji asisitiza utoaji wa elimu ya utunzaji mto mara kwa wanafunzi

News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kusisitiza utoaji wa elimu kwa wanafunzi ili kuwezesha elimu endelevu ya utunzaji wa mazingira ya Bonde la Mto Mara. Wito huo ameutoaMjini Butiamaakizindua maadhimisho ya Siku ya Mto Mara.

Ameitaka jamii kushirikiana katika kudhibiti uvuvi haramu na uchafuzi wa maji ili kuulinda na kuuendeleza Mto Mara ambao ni tegemeo kubwa la maji ya kunywa kwa binadamu, kilimo, Wanyama, uvuvi na shughuli nyingine za kijamii na uchumi.

“Tunahitaji kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa mlinzi wa Mto Mara kuanzia mtoto wa shule hadi mfugaji na mkulima. Tuimarishe elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi shuleni, tuhimize matumizi endelevu ya ardhi, tushirikiane kudhibiti uvuvi haramu na uchafuzi wa maji, na tuwe mstari wa mbele kuripoti uharibifu wa mazingira.” Amesema Mhandisi Mwajuma

Amesisitiza kuwa Mto Mara ni chanzo cha maisha kwa maelfu ya watu na viumbe hai. Uharibifu wa Mto Mara ni kujiangamiza. Kuhifadhi Mto Mara ni kuhifadhi maisha ya sasa na ya baadae.

Amesema ziko baadhi ya baadhi ya changamoto kubwa zinazoukabili Mto Mara ambazo ni pamoja na uharibifu wa misitu kandokando ya mto, uchimbaji wa madini usiozingatia sheria, pamoja na uchafuzi wa maji unaotokana na shughuli za kibinadamu hivyo ushirikiano kati ya serikali, Jamii, Asasi za Kiraia, na Wadau wa Kimataifa, kutawezesha kugeuza changamoto hizi kuwa fursa na kupata mafanikio.

Ameongeza kuwa maadhimisho ya siku ya Mto Mara ambayo hufanyika kila mwaka Septemba 15 ni tukio lenye fahari kubwa kwani linatoa fursa ya kutafakari juu ya umuhimu wa Mto Mara unaotiririka kutoka milima ya Mau nchini Kenya kupitia Hifadhi za Masai-Mara na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na hatimaye kuingia Ziwa Victoria.

Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara mwaka 2025 yanakwenda na kaulimbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara. Linda Uhai