Wasifu

Mteki Chisute

Mkurugenzi Huduma za Ubora wa Maji

Mteki Chisute

Mteki Chisute amezaliwa mwaka 1979, jijini Dar es Salaam. Amesoma Elimu ya Msingi katika Shule ya Mburahati, Wilaya ya Kinondoni kuanzia 1988-1994. Amepata Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Azania , Wilaya ya Ilala mwaka 1995 -1998 na Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Pugu mwaka 1999-200. Ana Shahada ya Usimamizi na Sayansi ya Mazingira (BSc Environmental Sciences and Management) kutoka Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), mkoani Morogoro alioyoipata mwaka 2002-2005. Mwaka 2009 alijiunga na Chuo cha Utafiti cha Maliasili (Institute of Natural Resources Assessment), Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili ya Usimamizi na Utafiti wa Maliasili, baadaye kujiunga na Chuo cha Greenwich/Saxion University of Applied Sciences in Deventer, Uholanzi kusomea
Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mazingira mwaka 2012.

Aliajiriwa na Wizara ya Maji kama Mkemia na kupangiwa kituo cha kazi katika Maabara ya Ubora wa Maji katika Kanda ya Mwanza mwaka 2006 na baadaye kuwa Mkuu wa Kanda hiyo kwa muda mfupi kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi Kutathmini Ubora wa Maji na Viwango mwaka 2021 akiwa na jukumu la kuhakikishaubora wa viwango vya maji yanayozalishwa kwa matumizi katika Idara ya Ubora waMaji, Wizara ya Maji Makao Makuu, Dodoma.