Miradi ya Kitaifa

Mradi wa Chalinze

Utekelezaji wa mradi wa Chalinze ulianza mwaka 2001 ukiwa na lengo la kuwapatia watu 105,000 maji safi na salama ifikapo mwaka 2015. Ujenzi wa mradi huo ulikamilika mwaka 2003, lengo ni kuvipatia huduma ya maji vijijini 20. Mradi huo ulifadhiliwa na Serikali ya China kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Awamu ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya vijiji 18 baada ya kukamilika kwa mradi. Vijiji vilivyokuwa katika awamu ya kwanza ni Chalinze, Pingo, Msoga, Mboga, Lugoba, Saleni, Mazizi, Msata na Kihangaike kwa upande wa Kusini. Upande wa Kaskazini, vijiji vilivyokuwemo ni Mandera, Hondogo, Kilemela, Miono, Kikaro, Rupungwi, Kimage na Mbwewe. Utekelezaji wa mradi huo uko katika awamu ya pili na unaendelea.

Mradi wa Handeni

Mradi wa Maji wa Handeni uko katika Wilaya Korogwe, katika Mkoa wa Tanga, ukiwa na eneo la kilometa za mraba 5000. Kilometa 316 ni truck main, kilometa 100 ni matawi ya mradi, vituo vya pampu sita, matanki ya kuhifadhi maji 56, vituo vya kuchotea maji 163, na waliunganisha mitandao ya maji 703. Mradi unahudumia vijiji 79 ukiwemo mji wa Handeni wenye idadi ya watu 180. Mradi huu una matoleo mawili kutoka Mto Pangani na kuyasukuma kwa kutumia nguvu za mtiririko asilia au nguvu za mashine. Toleo la Mandela (Tabora) linapeleka maji katika mtambo wa kusafisha maji wa “Slow Sand Filltes” unaochukua kiasi cha 2300 m3 kwa siku na toleo la Mkumburu (Segera) linachukua kiasi cha 170m3 kwa saa (4,080m3 kwa siku).

Mradi wa Kahama Shinyanga

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia fedha za ndani kupitia Wizara ya Maji imetekeleza mradi wa kutoa maji toka Ziwa Victoria kwa ajili ya matumizi ya wananchi katika miji ya Kahama na Shinyanga na vijiji 58 vilivyo njiani na bomba kuu na migodi ya madini. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 242. Mradi huu unalenga kuwapatia majisafi na salama ya kutosha kwa sasa watu wapatao 450,000 kwa kusambaza kiasi cha mita za ujazo 80,000 kwa siku. Mradi unategemewa kuongeza usambazaji wa maji hadi kufikia mita za ujazo 120,000 kwa siku na kuwapatia maji watu wapatao milioni moja ifikapo mwaka 2025

Mradi wa Maswa

Mradi wa maji wa Maswa unahudumia wakazi wa Mji wa Maswa pamoja na vijiji vya Zanzuli, Malita, Buyubi, Dodoma, Hinduki, Mwadila, Mwabayanda na Mwasita. Tanki la kuhifadhi maji la mradi huo lina uwezo wa kiasi cha mita za ujazo 8,600. Urefu wa mtandao wa mabomba ni kilometa 78.


Mradi wa Makonde

Mradi huu unahudumia maeneo ya Newala, Tandahimba na vijiji 14 vya Kata ya Nanyamba Wilaya Mtwara vijijini katika Mkoa wa Mtwara. Mradi huo una hudumia wananchi wa Wilaya za Mtwara kwa upande wa Mashariki, Lindi kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Masasi kwa upande wa Magharibi na upande wa Kusini mwa Mto Ruvuma mpakani na Msumbiji. Eneo la Mradi ni zaidi ya 4020km za mraba na idadi ya watu wanaohudumiwa na mradi huo ni zaidi ya watu 408,578. Makadirio ya uwezo mradi ni kutoa mita za ujazo 23,840 kwa siku na kuhudumia idadi ya watu wapato 347,140.


Mradi wa Mgango/Kiabakari

Mradi wa Maji wa Mgango/Kiabakari/Butiama unasimamiwa na Bodi iliyoanzishwa tarehe 30/01/2004 na wajumbe wa Bodi waliteuliwa na Waziri wa Maji tarehe 15/05/2004. Mamlaka ilikabidhiwa rasmi kazi ya kuendesha mradi huu kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Mkoa tarehe 01/09/2004. Uwezo wa mradi huu ni kuwapatia maji watu wapatao 64,255 katika vijiji 13, kwa sasa ni watu 38,553 tu wanaopata maji kwa umbali usiozidi mita za ujazo 400 ambao ni asilimia 60 tu ya watu waliotarajiwa. Maji yanayosambazwa ni mita za ujazo 4,157 kwa siku wakati mahitaji halisi ni m3 5,576 kwa siku.Mradi wa Wanging'ombe

Mradi huu unaoendeshwa kwa nguvu za mtiririko wa asili. Ulijengwa miaka ya 1980 ulifadhiliwa na UNICEF iliyochangia kiasi cha dola za Kimarekani 5,486,000, na Serikali ya Tanzania iliyochangia kiasi cha Sh.15,000,000/= Mradi huu uko katika Wilaya ya Njombe katika Mkoa wa Iringa ukiwa na eneo la Kilomita za mraba 1000. Mradi una matoleo mawili ya maji ya Mbukwa na Mtilafu yenye uwezo wa lita milion 6.70 na 6.0. Mpaka sasa mradi unahudumia vijiji 60 vituo 574 vya jamii na vifuo 568 zimeunganishwa. Mradi una matanki 54 ya kuhifadhi maji yenye ujazo wa kati ya 50m3 na 150m3.