Habari
Ujenzi wa Mabwawa ya Taka Sumu Uzingatie Sheria na Usalama
Serikali imeendelea kusisitiza kuwa ujenzi na usimamizi wa mabwawa ya taka sumu lazima uzingatie kikamilifu Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji pamoja na kanuni za usalama ili kulinda mazingira na maisha ya wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa mwaka unaojadili usalama wa mabwawa, Mkurugenzi wa IUbora wa Maji kutoka Wizara ya Maji, Heri Chisute, amesema suala la usalama wa mabwawa halipaswi kuangaliwa kama utekelezaji wa sheria pekee, bali pia ni jukumu la kimaadili kwa jamii zinazotegemea mifumo hiyo kwa ustawi wao wa kila siku. Aliongeza kuwa kutozingatia viwango vya usalama kunaweza kusababisha athari kubwa za kimazingira, kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi Chisute Chisute amesema kuwa hadi sasa nchi ina zaidi ya mabwawa ya maji 700, huku idadi ya mabwawa maalum ya kuhifadhi taka sumu ikiwa zaidi ya 60, hivyo kuhitaji usimamizi makini, ukaguzi wa mara kwa mara na mpango madhubuti wa kukabiliana na majanga.
Mkutano huo umejikutanisha wataalamu kutoka Sekta za Umma na Binafsi kujadili mbinu bora za kuimarisha usalama wa mabwawa, sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu: “Tahadhari za Dharura za Kukabiliana na Majanga ya Mabwawa ya Maji na Taka Sumu.”

