Habari

Imewekwa: Apr, 23 2024

​Waziri Aweso awahakikishia ushirikiano Watumishi wa Sekta ya Maji

News Images

Waziri Wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amezindua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maji na kuwataka wahakikishe wanafanya kazi kwa upendo na ushirikiano ili kuleta mafanikio.

Amesema Sekta ya Maji imepiga hatua kubwa kutokana na ushirikiano ambao umejengwa na kukuzwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Saluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katikq kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji "kumtua mama ndoo ya maji" .

Amesema viongozi wa Sekta ya Maji wanatambua jitihada kubwa zinazofanywa na watumishi wa wizara katika kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inafikishwa kwa Watanzania na kwamba wataendela kuongoza kwa kuhakikisha mazingira ya kazi yanaendelea kuboreshwa kwa watumishi ili kupata matokeo.

Amesema yapo mafanikio mengi ambayo wizara inapaswa kujivunia na kwamba hayo yote yametokana na ushirikiano mkubwa ambao wanapaswa kuuendeleza baina yao katika ngazi zote

Baraza la Wafanyakazi limehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, (ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza) na Naibu Katibu Mkuu Bi. Agnes Meena ambao wote kwa pamoja wamewahakikishia wafanyakazi wataendela kuhakikisha kila mtumishi anapata haki yake na kuwekewa mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu ya kazi kwa ubora unaotakiwa.