Habari

Imewekwa: May, 27 2024

​Ujenzi bwawa la Farkwa kuanza Septemba 2024

News Images

Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Farkwa linalotarajia kuhudumia wananchi wa Jiji la Dodoma na Miji ya wilaya za Chemba, Bahi na Chamwimo unatarajia kuanza mapema mwezi Septemba 2024.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ambaye amewakilishwa na Mkurugenzi Sera na Mipango Wizara ya Maji Prosper Buchafwe kwenye Kikao cha Pili cha Kamati ya Uongozi (steering Committee) kilichofanyika kwenye Wizara ya Maji, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Amesema taratibu zote za Wizara ya Maji kuhakikisha ujenzi huo unaanza zinaendelea vizuri ambapo tarehe 26 Aprili, 2024Wizara ya Maji ilitangaza zabuni ya Kandarasi. Amesema Serikali inatambua mahitaji ya wananchi wa Jiji la Dodoma, Miji ya Chemba, Bahi na Chamwimo hivyo itahakikisha inasimamia ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.

Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma amesema ujenzi wa bwawa hilo pia unahusisha ujenzi wa mtambo wa kutibu maji ambao utawezeshauzalishajiwa maji lita milioni 128 kwa siku.

Aidha, ujenzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 hadi 2025.

Ujenzi wa Bwawa la Farkwa awamu ya kwanza unafanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Kwa gharama ya dola za marekani milioni 132.9