Habari

Imewekwa: Apr, 14 2023

​Naibu Katibu Mkuu Luhemeja ateta na watumishi wa Wizara

News Images

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya kikao na watumishi wa Wizara ya Maji makao makuu jijini Dodoma na kuwataka wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyopangwana Serikali katika kufikisha huduma ya maji mijini na vijijini.

Amesema sekta ya maji ni sekta muhimu na inabeba uhai wa binadamu hivyo kila mtumishi wa sekta ya maji anapaswa kufahamu kuwa amebeba matumaini makubwa ya jamii ya Watanzania.

Mhandisi Luhemejaamesema ni ukweli kuwa maji ni uhai namaji ni ibada ambapo serikali imepanga ifikapo mwaka 2025 huduma ya maji vijijini nchiniiwe imefika asilimia 85 na mijini huduma hiyo ikiwa imefika asilimia 95.

“Nina uhakika hili linawezekana na tunaweza kuvuka malengo hivyo sisi watumishiwa umma tuhakikishe tunatimiza wajibu wetu” Mhandisi Luhemeja amesema.

Amesema viongozi wa wizara wako tayari kuhakikisha changamoto zinazowakuta watumishi katika kufikia malengo zinapatiwa majibu na ufumbuzi hivyo wasijione wako pepe yako.

Kwa upande wao watumishi wa Wizara hiyo wamemshukuru Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Luhemeja kwa kuwa tayari kuwasikiliza na kuonesha utayari wa kutatua changamoto zinazowakumba.

“Nikuhakikishie sisi watumishi wa Wizara tuko tayari kufanikisha malengo. Tunaomba ufikishe salam zetu kwa Waziri Mhe. Aweso. Naibu Waziri Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi na Katibu Mkuu Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuwa sisi watumishi wa Wizara tunawaamini sana. Tunaimani na uongozi wao na tunahakikika kupitia uongozi wenu yote yatawezekana. Amesema Sospeter Bukwali mtumishi wa Wizara ya Maji.