Habari

Imewekwa: Sep, 08 2023

​Mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe watakiwa kuongeza kasi

News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe na kuwataka wakandarasi kukamilisha kazi hiyo mapema ili wananchi wanaotarajia kunufaika kupata huduma ya maji waipate mapema katika maeneo ya Same na Mwanga.

Prof. Jamal katika ukaguzi huo ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi ambao utatua changamoto ya muda mrefu za upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ratiba ya utekelezaji wa mradi na ikiwezekana kazi ifanyike na kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwasababu huduma ya maji ni haki ya msingi na Serikali imejipanga kufanikisha jambo hilo kwa wananchi.

Kiongozi wa Timu ya Uratibu wa Mradi Mhandisi Abbas Pyarali, amesema hadi tarehe 31 Agosti 2023 utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefika asilimia 79.5.

Kitengo cha Mawasiliano