Habari
Wizara ya Maji Yaendesha Mafunzo Kuhusu Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji - Kidakio cha Bahi
Wizara ya Maji kupitia programu ya Uhimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi na uboreshaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma imeendesha mafunzo ya usimamizi na uhifadhi wa kidakio cha Bahi ambacho ni chanzo cha maji cha mto Bubu unaotiririsha maji kuelekea eneo litakapojengwa bwawa la Farkwa.
Mafunzo yamefanyika mjini Babati, Manyara yakihusisha wadau wanaoishi katika kitakio cha Bahi upande wa juu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji anayesimamia Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji Bi. Rosemary Rwebugisa kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji amefungua mafunzo hayo.
Amesema utunzaji wa vyanzo vya maji ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uwepo wq huduma endelevu ya majisafi nchini.
Kuhusu Kidakio cha Bubu ni kuhakikisha bwawa la Farkwa linakuwa endelevu.
Amesema kidakio cha Bahi ni muhimu kutunzwa ili kuhakikisha Mto Bubu unaendelea kutiririsha maji yake mwaka mzima kuelekea maeneo jirani na kufika katika bwawa la Farkwa litakalojengwa wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.
Ameongeza tangu serikali iutangaze mji wa Dodoma kuwa mji mkuu wa serikali mahitaji ya maji yanazidi kuongezeka kwa kasi na kiwango cha uzalishaji hakiendani na kasi ya ongezeko la idadi ya watu kwasababu mahitaji ya maji kwa siku katika jiji la Dodoma yanakadiriwa kufika lita million 127 na uzalishajii ni liita milioni 88 kwa siku.
Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto ya ongezeko la huduma ya majisafi, ujenzi wa bwawa la Farkwa ni moja ya mkakati wa muda wa kati wa kukabiliana na mahitaji ya maji katika jiji la Dodoma.
Ameilekeza Bodi ya Maji ya Bonde la Kati ambayo ndio yenye jukumu la kusimamia Kidakio cha Bahi, kuandaa Mpango Jumuishi wa Uhifadhi wa Kidakio kwa kuzingatia ushauri wa mtalaam mshauri na kuwasilisha Wizara ya Maji.
Ili mradi ukamilike na kutoa matunda ni vema wananchi kuendelea kupewa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu Kando ya Vyanzo vya Maji kama vile kilimo na uvuvi, Ili kuendeleza uhai wa vyanzo hivyo.
Mratibu wa Mradi Mhandisi James Mallya, ametoa elimu kuhusu mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa ili kuwajengea uelewa wadau hao.
Ameahidi elimu kwa wadau kuhusu mradi ni endelevu. Amesema shughuli za ujenzi wa bwawa zitaanza baada ya wafadhili ambao ni Bank ya Maendeleo ya Afrika ( AfDB) kuridhia na kutoa kibali cha kuendelea na hatua ya ujenzi.
Kitengo cha Mawasiliano

