Habari

Imewekwa: Feb, 18 2024

Kamati ya Bunge ya PAC yaipa tano Wizara ya Maji kuhusu Jengo la Ofisi Dodoma

News Images

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imekagua jengo jipya la Wizara ya Maji katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na kutoa pongezi kwa ujenzi wa jengo la kisasa na lenye kutosha watumishi wote.

Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Ujenzi waJengo hilo unathamani yashilingi bilioni 24.1 fedha za ndani, likiwa na ghorofa sita, vyumba 281 vyenye uwezo wa kuhudumia watumishi wasiopungua 350. Piakumbi 12 za mikutano.

Kamati hiyo imeridhishwa na ubora wa jengo. Imeipongeza serikali kwa kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma na kuwataka watumishi wa Wizara kuhakikisha wanajituma ili kuleta matokeo na majibu kwa jamii katika utendaji kazi wao.

Jengo hilo limekamilika na kukabidhiwa kwa wizara ambapo watumishi wa wizara hiyo tayari wamehamia tangu Januari 2024.