Habari
Imewekwa:
Nov, 17 2022
Dkt. Mpango awataka wataalam kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameshudia uwekwaji saini wa azimio la Mbeya katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Upandaji Miti Rafiki wa Maji na Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde uliofanyika jijini humo.
Azimio hilo lilisainiwa na Mawaziri wa sekta mtambuka na linalenga kuhifadhi, kutunza na kuendeleza rasilimali za maji.
Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo Mhe. Mpango amewataka viongozi wa Vyama vya Siasa na Wataalamu wa sekta zote kusimamia kikamilifu, kuweka mipaka, na kuwaondoa wananchi waliojenga maeneo ya milimani kwa kuwapatia maeneo mengine.