Habari
Bodi ya kwanza ya RUWASA yazinduliwa

TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) leo amezindua Bodi ya kwanza ya Wakurugenzi wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) jijini Dodoma.
Mhe. Prof. Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuisimamia vyema RUWASA ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa kuondoa changamoto ya huduma ya maji hasa katika kutekeleza miradi ya maji vijijini.
“Zipo changamoto ikiwamo usanifu wa miradi, na gharama za ujenzi wa miradi zinazotolewa na wakandarasi”, Prof. Mbarawa amesema.
Waziri Mbarawa amesema kasi ya utendaji kazi ya RUWASA lazima iongezeke na kuiagiza bodi aliyoizindua kufanya maamuzi na kutoa ushauri kwa wakati ili kutatua changamoto zinazojitokeza.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya RUWASA ni kama ifuatavyo:
1. Prof. Idrissa Mshoro- Mwenyekiti
2. Mhandisi Clement Kivegalo- Katibu
3. Mhandisi Ngwisa Mpembe- Mjumbe
4. Mhandisi Amos Maganga- Mjumbe
5. Bw. Salehe Njaa- Mjumbe
6. Bi. Grace Chitanda- Mjumbe
7. Mhandisi Nadhifa Kemikimba- Mjumbe
8. Prof. Evelyne Mbede- Mjumbe
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini