Habari

Imewekwa: Sep, 04 2023

​Aweso asisitiza kupata majibu na kutatua changamoto za Sekta ya Maji kwa wakati

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka watumishi wa Sekta ya Maji kuhakikisha wanatatua changamoto za sekta hiyo kwa haraka na kwa wakati. Ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji na watumishi wa taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo.

Amesema lengo laWizara ya Maji ni kuhakikisha inaendelea kuwa wizara bora kwa kutoa huduma ya maji kwa wanachiili kuleta maendeleo nchini.

“Niwatake wote mkatekeleze majukumu yenu. Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuamini na kuendelea kutuweka pamoja katika wizara hii, hivyo tushirikiane sisi watumishi, twendeni tukafanye kazi ili kuhakikisha malengo yetu yanafikiwa” Aweso amesema

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesemaweledi na kasi katika utekelezaji wa miradi ya maji inatoa mwanga na mwelekeo mzuri katika kila kona ya nchi, hivyo juhudi hizo ziendelee zaidi, na kuwashirikisha wananchi pale wanapohitaji kwani ndio wanufaika wakubwa na wadau wa Serikali katika miradi ya maji.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu aliyeteuliwa katika wadhifa huo hivi karibuni amekaribishwa katika familia yawatumishi wa Sekta ya Maji, na ameahidi kuwa kiongozi wa kusukuma maendeleo mbele zaidi ili kufikia malengo ya nchi.

Amesema kushirikiana na kutatua changamoto kwa pamoja kutahakikisha huduma ya maji kwa kila Mtanzania inatimiia kwa wakati na ziada pia kwakufikisha maji vijijini kwa silimia 85 na mijini kwa asilimia 95.

“Kila mmoja katika nafasi yake ahakikishe analenga kwenda zaidi ya hapo” Prof. Katundu amesema.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Mwajuma Juma amesema maendeleo yote yaliyopatikana katika Sekta ya Maji yamebebwa na ushirikiano wa dhati kati ya Watumishi na Viongozi.

Mhandisi Mwajuma ambaye naye ameteuliwa hivi karibuni katika nafasi hiyo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha Watanzania wote wanapata majibu ya uhakika kuhusu huduma ya maji, na huduma hiyo inakuwa endelevu katika makazi yao.

Kitengo cha Mawasiliano