Wasifu

Kaimu Mkurugenzi, Ufuatiliaji na Tathmini
Diana F. Kimario
Diana Focus Kimario anafanya kazi za ufuatiliaji na tathminiwa utekelezaji wa Sera, Mpango Mkakati wa Muda wa Kati, mipango ya mwaka, bajeti, programu na miradi inayotekelezwa na Wizara. Vilevile, anafuatilia utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara; kuandaa taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya maeneo muhimu ya masuala ya Kitaifa (National Key Results Areas); pamoja na kuwa mwangalizi wa takwimu za Wizara.
Bi. Kimario ana Shahada ya Uzamili (Masters of Arts specializing in Statistics) kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelors of Science with Computer Science) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya kuteuliwa kwake, amefanya kazi katika Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Maji na ana uzoefu na utaalamu wa kuandaa na kutekeleza Sera, mipango mikakati, mipango ya mwaka, bajeti, programu na miradi inyotekelezwa na wizara. Amekuwa ni afisa katika madawati mbalimbali ikiwemo la uratibu wa usimamizi wa vihatarishi (Risks Coordinator) katika Wizara. Kabla ya kujiunga na Wizara ya Maji alifanya kazi na Kampuni ya KAJIMA kama afisa anaeshughulikia masuala ya kompyuta.