Chuo Cha Maji

Chuo cha Maji kina jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalamu wanaotumika na wanao tarajia kutumika katika sekta ya maji, mafunzo yamejikita katika masuala ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira. Mafunzo yanatolewa kwa muda mfupi na muda mrefu. Bofya hapa kusoma zaidi

Majukumu
Majukumu ya Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji ni kama ifuatavyo:

  • Kutekeleza shughuli za kiutawala na nyinginezo ili kupata ufanisi katika kutoa mafunzo;
  • Kufundisha wataalamu, mafundi sanifu, mafundi bomba kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya maji;
  • Kuboresha mitaala na kutengeneza vitendeakazi kwa ajili ya kufundishia karakana na
  • Kutunga na kusimamia mitihani na kuhakikisha hakuna uvujaji wa mitihani.