Habari
Aweso ampa siku 30 mkandarasi kuthibitisha uwezo wake

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametoa Mwezi mmoja kwa mkandarasi wa mradi wa maji wa miji 28 mjini Kasulu kampuni ya Megha Engeneering & Infrastructures LTD kuthibitisha utayari wake wa kukamilisha mradi kwa wakati.
Aidha amemuweka chini ya uangalizi wa Mkuu wa mkoa wa Kigoma na wasimamizi wengine wa sekta ya maji kujiridhisha iwapo amejipanga na anao uwezo wa, kutekeleza mradi kwa wakati.
Kwa mjibu wa Mkataba mradi huo umepangwa kukamilika Oktoba 10, 2025 na hadi sasa umefika asilimia 49 ya utekelezaji.
Waziri Aweso amechukua hatua baada ya kupata majibu ya mkandarasi kuwa hana changamoto yoyote anayokutana nayo kutoka serikalini ikiwemo malipo ya kazi.
Amesema kasi ya utekekezaji hairidhishi hali ambayo inatishia kuchelewesha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.
Amesema mradi huo unatekekezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 35 na mkandarasi amekuwa akilipwa kwa wakati
Amesema hadi Septemba 2025 Wizara ya Maji itafanya tathmini kuona utayari wa mkandarasi na kuchukua hatua muhimu ili kufanikisha huduma ya majisafi kwa wananchi
Mradi wa Maji wa Miji 28 mjini Kasulu unatarajia kuzifikia kata 13 kati ya 15 za wilaya ya Kasulu.