Bodi za Maji za Mabonde

Bonde la Kati

Bonde hili linajumuishwa na Mito na Vijito vinavyoingiza maji yake katika Ziwa Ambali linapatikana katika Kanda ya Kati ya Kaskazini. Vijito vidogovidogo vinavyotoka Ziwa Natron mpakani mwa Kenya kuelekea Tanzania kwenye bonde la Bahi. Eneo la bonde kwa upande wa Tanzania ni kilometa za mraba 153800. Maziwa makuu inayomwaga maji katika bonde hili ni Ziwa Eyasi linalopokea maji kutoka katika Mto Wembere na Manonga iliyopo Kaskazini mwa Tabora na Mashariki mwa Shinyanga. Ziwa Manyara hupokea maji yake kutoka kwenye ardhi chepechepe ya Bubu. Maziwa mengine madogo yaliyopo katika bonde hili ambayo hayamwagi maji yake nje ni ziwa Basuto na Natron. Bonde hili liko katika maeneo kame ya Tanzania, ambapo wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya 500 Milimita katika maeneo ya Bahi na 900 Milimita katika vilima vya Mbulu.

Bonde la Ziwa Tanganyika

Bonde la Ziwa Tanganyika liko Magharibi mwa nchi ya Tanzania, Bonde hili linajumuisha mabonde yote madogo yanayomwaga maji yake katika ziwa Tanganyika. Bonde lina ukubwa wa kilometa za mraba 239,000 na ukubwa wa ziwa lenyewe ni kilometa za mraba 32,000. Eneo la ardhi kwa upande wa Tanzania ni kilometa za mraba 151,000 ni sawa 60% ya maji yanayoingia ziwa Tanganyika. Sehemu kubwa ya bonde ni Mto Malagarasi yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 130,000.

Mto Malagarasi umeanzia katika maeneo ya milima ya mpakani mwa Burundi na Tanzania katika muinuko wa 1750 kutoka usawa wa bahari. Mto unateremka Kaskazini mashariki kupitia kwenye vilima na miteremko kuelekea kwenye ardhi chepechepe ya Malagarasi. Vijito vikuu vya mto Malagarasi ambavyo ni Myowosi na Igombe vinakutana katika Ziwa Nyamagoma. Mito ya Ugala na Ruchungi inakutana na mto Malagarasi upande wa chini wa Ziwa Nyamagoma, Kwa upande wa Magharibi unapita kwenye majabali ya Misito ambapo yanatengeneza maporomoko kabla ya kuingia Ziwa Tanganyika. Mto Ugala unapokea maji kutoka katika eneo la kilometa za mraba zipatazo 52,000 na kabla haujakutana na mto Malagarasi unapita katika maeneo oevu na kutengeneza Ziwa la muda la Ugala na Sagara.

Vijito vingine vikubwa ni Ruchungi unaopokea maji kutoka vilima vya kaskazini vya Kasulu kuelekea upande wa kusini na kupitia katika maeneo oevu kabla ya kuingia mto Malagarasi maeneo ya Uvinza. Pamoja na mto Malagarasi Ziwa Tanganyika pia linapokea maji kutoka katika mabonde madogo madogo, upande wa kaskazini Magharibi wa Kigoma kuna mto Luiche, ambao hufurika wakati wa mvua.

Bonde la Wami Ruvu

Bonde le wami Ruvu linajumuisha mito mikuu miwili ambayo ni Wami wenye kilometa za mraba 400000 na Ruvu kilometa za mraba 17700. Pamoja na mito ya ukanda wa Pwani iliyopo Kusini mwa Dar es salaam. Bonde hili kwa ujumla linaukubwa km za mraba 72930 pia lina maeneo ya tambarare na safu ndefu za milima.
Kuna aina nne za milima katika bonde hili ambazo ni:

Milima ya Uluguru iliyopo Kusini Mashariki (altitude 400 mpaka 2500m

Milima ya Nguru iliyopo Magharibi ya Kilosa (altitude 400 mpaka 2000m)

Milima ya Rubeho iliyopo Magharibi ya Kilosa (altitude 500 mpaka 1000m)

Milima ya Ukaguru iliyopo Kaskazini mwa Wami (altitude 400 mpaka 1000m)

Bonde la Ziwa Victoria

Bonde la Ziwa Victoria ndani yake kuna Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa kuliko yote Barani Afrika na chanzo cha mto White Nile. Ziwa Victoria lipo katika Latitudi 031 Kaskazini na 354 Kusini, na Longitudi 3118 Mashariki na 3454 Magharibi. Lina wastani wa kina cha mita 80. Ziwa hili linajumuisha nchi 3 ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda. Mito ambayo inamwaga maji Ziwa Victoria ni pamoja na Mto Kagera, Simiyu, Mbarageti, Gurumeti, Mara na Mori. Upande wa Mashariki wa bonde hasa katika miinuko ya Tarime, misimu ya mvua ni miwili, wakati upande wa Kusini wa bonde ambao ni mkoa wa Mwanza kuna msimu wa mvua na kiangazi, na upande wa Magharibi unapata mvua kipindi chote cha mwaka na mvua chache katika mwezi wa saba. Kiasi cha wastani wa mvua kwa mwaka kinatofautiana katika maeneo mbalimbali ya ziwa na maeneo yanayolizunguka. Upande wa Mashariki wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya 500 na 700mm. Upande wa Magharibi mvua huongezeka hadi kufikia wastani 2000mm katika maeneo ya Bukoba na visiwa vya Ssese. Upande wa kusini mwa ziwa katika maeneo ya Mwanza wastani wa mvua ni kati ya 750-1100mm na upande wa Mashariki katika maeneo ya Mara wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya 750-1000mm na huongezeka hadi 1600mm katika miinuko ya Tarime.

bofya hapa kwa taarifa zaidi


Bonde la Mto Ruvuma

Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini lina mito mikuu mitano inayomwaga maji yake katika bahari ya Hindi. Mito hiyo ni Mto Matandu wenye kilometa za mraba 18,565, Mto Mavuji wenye kilometa za mraba 5,600, Mto Mbwemkuru wenye kilometa za mraba 16,255, Mto Lukuledi wenye kilometa za mraba 12950 na vijito vya mto Ruvuma Maeneo ya mabonde madogo yapo kati ya altitudi 305-710 juu ya usawa wa bahari, na hutiririsha maji yake kuelekea ukanda wa pwani. Mto Ruvuma unashirikiana kati ya Tanzania na Msumbiji na unamwaga maji yake katika bahari ya Hindi. Mto huu una urefu wa kilometa 800 kati ya hizo kilometa 650 zipo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Bonde la mto Ruvuma lina ukubwa wa kilometa za mraba 152,200 kati ya hizo kilometa 52,200 (34.3%) zipo Tanzania na kilometa 99,530 (65.39%) zipo Msumbiji na Malawi kilometa 470 (0.31%). Vijito vikubwa vya mto huu kwa upande wa Tanzania vimeanzia katika wilaya za Mbinga, Tunduru na Masasi. Wastani wa maji yanayoingia mto Ruvuma kwa mwaka ni mita za ujazo 15,000 milioni. la mto Ruvuma na pwani ya kusini lina ukubwa wa kilomita za mraba 104,270 na idadi ya watu wapatao 2,241,944. Wastani wa nyuzi joto ni 260C kwa ukanda wa pwani na nchi kavu nyuzi joto 24, mabadiliko ya hali ya joto kwa siku na mwaka hutokea

Bonde la Mto Rufiji

Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji inayosimamia matumizi ya maji katika Bonde la Rufiji. Bonde hili maana yake ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake huingia Mto Rufiji na hatimaye Bahari ya Hindi. Bonde hilo lina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 177,420 na lina mito mikuu minne ambayo ni Great Ruaha Mkuu wenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 82,970, Kilombero wenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 39,990. Mto mwingine ni Luwegu wenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 26,300 na Mto Rufiji wenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 22,160. Ofisi ya Bonde la Rufiji iko katika Mkoa wa Iringa barabara ya Dodoma. Kimuundo ofisi hiyo iko chini ya Idara ya Rasilimali za Maji katika Wizara ya Maji. Hutekeleza malengo yake kwa kushirikiana na ofisi za Halmashauri za Wilaya zote zilizoko kwenye Bonde hilo. Bonde hilo lina Bodi yake ambayo ina wajumbe kumi ambapo Afisa Maji wa Bonde ndiye Katibu wa Bodi hiyo. Bodi na ofisi ya Bonde la Rufiji ilianzishwa Septemba 1993, kwa mujibu wa Sheria ya Maji Na.42 ya mwaka 1974 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1981 na 1991. Aidha, Waziri mwenye dhamana ya rasilimali za maji ndiye mteuzi wa Bodi hiyo.

Bonde la Ziwa Nyasa

1.1 Utangulizi

Bonde la Ziwa Nyasa ni eneo lote ambalo mwelekeo wa maji yake kuanzia kwenye vidaka maji, chemichemi, vijito na mito, na kutiririsha maji yake katika Ziwa Nyasa.

Bodi ya Maji ya ya Bonde la ziwa Nyasa ilianza shughuli zake rasmiJulai 14, 2002 Jijini Mbeya, na mwaka 2010ofisi ilihama kutoka Mbeya mjini kwenda Tukuyu mjini ambapo ndiyo makao makuu ya ofisi; pia kuna ofisi ndogo Songeamjini.

Bonde la Ziwa Nyasa linajumuisha mikoa mitatu na wilaya kumi na tatu , ambazo ni mkoa wa Mbeya (wilaya za Rungwe, Mbeya vijijini, Mbozi, Ileje, Momba na Kyela); Mkoa wa Njombe (Wilaya za Makete, Njombe na Ludewa); Mkoa wa Ruvuma (Wilaya za Songea, Namtumbo, Mbinga na Nyasa).

Hivyo Bonde la Ziwa Nyasa linaunganisha maeneo kutoka katika mito ya Songwe, Kiwira, Lufilyo, Mbaka, Nkiwe, Mchuchuma, Ruhuhu, Mwinamaji, Mbawa, Luhekei, Ruhuhu na mto Chiwindi.

Kuna maziwa madogo ya asili (Crator lakes) katika wilaya ya Rungwe pekee mbayo ni Kisiba, Kitubwi, Kyambangunguru, Ilamba, Kingiri, Itenda, Kyungururu, Itamba, Kyejo na Ngozi.

Bonde la ziwa Nyasa linaunganisha nchi tatu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Malawi na Jamhuri ya Msumbiji. Utafiti uliofanyika umebaini kuwa zaidi ya asilimia mia 59 ya maji yote yanatoka Tanzania, Malawi inachangia asilimia 33 na Msumbiji inachangia asilimia 8.

Bonde la Ziwa Nyasa (Tanzania) lina asilimia 2 katika Bonde la Mto Zambezi (ZAMCOM) linalounganisha nchi nane ambazo ni Msumbiji, Angola, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Namibiana Tanzania . Pia maji kutoka Ziwa Nyasa kupitia mto Shire ulioko MalawikatikaBonde la mto Zambezi, Tanzania inachangia asilimia 11.3.

2.1 Majukumu ya Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Nyasa

i) Kusimamia na kuratibu matumizi yote ya rasilimali ya maji yaliyo juu ya ardhi na yaliyo chini ya ardhi.

ii) Kutoa hati ya haki ya matumizi ya maji

iii) Kudhibiti matumizi ya maji kipindi cha Kiangazi

iv) Kudhibiti uchafuzi wa maji na vyanzo vya maji

v) Kufanya utafiti unahusiana na matumizi ya maji

vi) Kushirikiana na wadau kutatua migogoro ya matumizi ya maji

vii) Kusimamia ukusanyaji wa ada ya matumizi ya maji kila Mwaka

viii) Kushirikiana na Watumia Maji kuunda Vyama vya Watumia Maji

ix) Kutoa Elimu juu ya Matumizi Bora ya Rasilimali Maji na Hifadhi ya Mazingira.

x) Kushirikiana na watumia maji katika kulinda, kutunza, kusimamia na kuhifadhi vyanzo vya maji na mazingira.

2.3 Jiografia

Kwa wastani kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya mm 1000 hadi mm 2500, hali ya hewa inatofautiana sana kati ya maeneo yanayozunguka Ziwa Nyasa na milima ya Rungwe na Livingstone.

Wastani wa mwinuko ni kati ya Meta 500 hadi 2500 kutoka usawa wa bahari, na joto ni kati ya nyuzi 10 hadi 25 katika vipimo vya Celcius.

2.4 Shughuli za Uchumi kwa Wakazi katika Bonde

Wananchi zaidi ya asilimia 80, wanaoishi katika eneo la Bonde la Ziwa Nyasa wanajishughulisha na kilimo cha mazao ya ya biashara kama chai, kahawa, na pareto. Mazao ya chakula kama viazi vitamu na viazi mviringo, mpunga, mahindi, maharage, nganona njegere. Wananchi wanaoishi kandokando ya Ziwa Nyasa wanajishughulisha na uvuvi.

2.5 Matumizi ya Maji

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji mtu yeyote anayetumia maji kwa kujengamiundo mbinu katika chanzo cha maji anapaswa awe na kibali cha matumizi ya maji na anapaswa kukilipia kila mwaka.

2.6Tathmini ya Rasilimali za Maji

Ili kupanga mipango ya uhakika kuhusu matumizi ya maji katika eneo lolote, inahitajika kuwa na taarifa sahihi juu ya kiasi cha maji yaliyopo juu na chini ya ardhi.

Taarifa hizi tunazipata katika vituo mbalimbali vilivyojengwa katika maeneo mbalimbali katika Bonde. KatikaBonde kuna jumla ya vituo 34 vinavyopima wingi wa maji mitoni, vituo vitatu (3) vinavyopima wingi wa maji Ziwani na vituo20 vinavyopima mwenendowa mvua; ambavyo vimekarabatiwa na kujengwa kupitia Mradi wa Kuendeleza Sekta ya Maji, Awamu ya Kwanza (WSDP I).

Maji chini ya ardhi hayajaguswa sana kutokana na eneo la bonde kuwa na maji mengijuu ya ardhi, japo kuna visima virefu vichache katika wilaya zote.

2.7 Hali ya Vyanzo vya Maji

Bonde la Ziwa Nyasa ni bonde ambalo lina maji mengi ukilinganisha na mabonde mengine hapa Tanzania; lina wastani wa mvua upatao 1500mm hadi 2800mm kwa mwaka. Bonde hili lina vyanzo vya maji aina mbalimbali kama chemichemi, ardhi oevu, Mito, Maji chini ya ardhi nk. Mito mikubwa katika Bonde la Ziwa Nyasa ni pamoja na Ruhuhu, Songwe, Kiwira, Mbaka, Rufirio, Nyitule, Lumbira, Nkiwe, Mchuchuma, Luhekei, Mbawa, na Mwinamaji. Mito yote hiyo inatiririsha maji kipindi chote cha mwaka. Baadhi ya Matumizi ya Maji katika Bonde la Ziwa Nyasa ni pamoja na Matumizi ya Nyumbani, Umwagiliaji, Uzalishaji wa Umeme, Uchakataji wa Madini, Uvuvi na Usafirishaji.

2.8 Maji Shirikishi

Bonde la Ziwa Nyasa lina maji shirikishikama ifuatavyo:

  • Ziwa Nyasa linazishirikisha nchi nane za Tanzania, Msumbiji,Malawi, Zambia,Zimbabwe,Botswana, Angola na Namibia.
  • Mto Songwe ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Malawi Kusini Magharibi mwa Tanzania.
  • Mto Chiwindi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji Kusini mwa Tanzania.

NA

MAELEZO

KIASI CHA MAJI

Meta za ujazo milioni kwa Mwaka

1.

Mito ya Tanzania inaingiza Mita za ujazo milioni kwa Mwaka:

  • Ruhuhu:94,290
  • Songwe:12,734
  • Kiwira:64,195
  • Lufyrio:21,559
  • Lumbira:11,162
  • Mbaka:10,904
  • Mito mingine midogo: 16,953

231,797 (59%)

2.

MAJI TUNAYOTUMIA UPANDE WA TANZANIA.

Maji yanayotumika kwa ajili ya maji majumbanitu (Domestic Water Supply)ni Mita za Ujazo million 35.97 kwa mwaka.

35.97(27.9%)