Habari

Imewekwa: Nov, 22 2022

Waliochepusha maji sasa ni kilio

News Images

Wataalam wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar wameungana na wenyeji wao wa Wizara ya Maji Tanzania bara kutembelea Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa lengo la kujifunza na kushirikishana namna bora ya utunzaji ugawaji na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Ziara hiyo inafanyika kufuatia makubaliano ya wizara hizi mbili za pande mbili za Muungano katika kuhakikisha wanashirikishana namna bora ya kutatua changamoto zinazazoikumba sekta ya maji kwa kila upande.

Wataalam hao wameanzia ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Rufiji mkoani Iringa ambapo Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Frolence Mahay amesema Bodi imerejesha uelekeo wa maji ya mito ambayo ilikuwa imezuiwa na kuta zilizokuwa zimejengwa na wakulima na wafugaji sehemu mbalimbali. Kuta hizo zilikuwa zikielekeza maji mashambani na hivyo kuzuia maji kutiririka katika mkondo wake jambo ambalo lilikuwa likiathiri Maisha ya viumbe hai na shughuli mbalimbali za kijamii upande wa pili wa mto.

Amesema serikali imeweka utaratibu wa kuomba kibali cha kutumia maji lakini watumiaji hao walikuwa wakiyatumia maji hayo kinyume na utaratibu na hivyo.

Aidha, amesisitiza watumiaji wa maji wahakikishe wanapata vibari vinavyowaruhusu kutumia maji hayo.