Habari
Wakandarasi wenye Sifa Ndiyo Watakaopata Kazi za Miradi ya Maji

Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amesema wakandarasi wenye sifa na uadilifu ndiyo watakaopata kandarasi za ujenzi wa miradi miradi ya maji.
Waziri Mbarawa amesema hayo leo wakati akizindua mradi wa maji wa Nchinila uliogharimu kiasi cha shillingi milioni 438. Mradi huo umejengwa katika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
“Wakandarasi wanaoweka bei kubwa katika miradi ya maji na kujenga miradi isiyokuwa na viwango serikali haitawavumilia na hawatapata tena kazi”, Prof. Mbarawa alisema.
Pamoja na uzinduzi huo, Waziri Mbarawa amebaini mkandarasi wa kampuni ya Kwilasa iliyopewa kandarasi ya mradi wa maji wa Kazingumu haifanyi kazi kwa kiwango kuendana na mkataba ingawa imeshalipwa kiasi cha shilingi milioni 56.
Waziri Mbarara ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kufuata utaratibu ili kuvunja mkataba na Kampuni ya Kwilasa katika ujenzi wa mradi wa maji wa Kazingumu.
Waziri Mbarawa amemaliza ziara ya kikazi mkoani Manyara kwa kukagua miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Simanjiro na Kiteto.
Kitengo cha Mawasiliano
3 Septemba, 2019