Habari

Imewekwa: Nov, 24 2023

Tuwe wazalendo na miradi yetu - Mhe. Majaliwa

News Images

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amezitaka Taasisi na Mashirika ya Umma kote nchini yanayotekeleza miradi mbalimbali kuwa na uzalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Mhe. Majaliwa amesema hayo ikiwa ni matokeo yakutekelezwa kwa weledi, ufanisi, kiwango na uzalendo mkubwakwa Mradi wa Maji wa Itumba-Isongole wilayani Ileje, mkoa wa Songwe, ambapo Leo tarehe 23 Novemba, 2023 ameweka jiwe la msingi la mradi huo.

Mhe. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ((Mb) na Naibu wake, Mhe. Mhandisi MarypriscaMahundi (Mb) pamoja na wataalamu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa usimamizi mzuri wa fedha za mradi wa maji wa Itumba-Isongole na kutekeleza mradi huo kwa gharamaya shilingi bilioni 2.6 kati ya bilioni 4.9 ambazo zilitengwa ili kutekeleza mradi huo, hivyokubaki kwa fedha ya serikaliambayo itatekeleza miradi mingine ya maji, na kwamba ni vema watekelezaji wa miradi ya serikali wakajenga utamaduni wa uzalendo na uadilifu katika matumizi ya fedha za umma.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Mary Prisca Mahundi (Mb) amemuwakilisha Waziri wa Maji, katika ziara hiyo ya siku nne mkoani Songwe kuanzia tarehe 22 -25 Novemba, 2023.

Mhe. Godfrey Kasekenya, Mbunge wa Jimbo la Ileje ameipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa mradi wa maji wa Itumba-Isongole ambao utaondoa kabisa tatizo la hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 100 wilayani Ileje na kuwa na ziada ya maji.

Mradi wa Maji wa Itumba-Isongole katika Wilaya ya Ileje, mkoani Songwe unatekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023 na utahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini wa miji ya Itumba na Isongole wilayani Ileje.