Habari

Imewekwa: Sep, 19 2023

​Serikali yaahidi kutoa milioni 500 kusambaza maji mjini Lindi

News Images

Wizara ya Maji imeahidi kutoa shilingi milioni 500 ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kwa wananchi wa Lindi Mjini. Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) mbele ya Rais Samia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mitwero Mjini Lindi.

Amesema utekelezaji wa mradi wa Ng'apa umewezesha uzalishaji mkubwa wa maji na hivyo kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi wa Lindi.

Aidha, Mhe. Aweso amekili kuwepo na changamoto ya miundombinu ya usambaji maji kwani mahitaji ya maji kwa watu wa Lindi ni lita za ujazo milioni 7 kwa siku wakati uzalishaji ni zaidi ya milioni 10

"Nimuahidi Dada yangu Hamida Abdallah. Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini kuwa ndani ya wiki hii wizara italeta milioni 500 ili wananchi wa Lindi wasambaziwe maji" Aweso amesema.

Awali akitoa salam za wananchi wa jimbo la Lindi mjini Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Hamida Abdalah aliomba serikali iwezeshe ujenzi wa miundombinu ya maji kwa wananchi kwani uhitaji ni mkubwa. Mhe. Hamida amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wananchi wa jimbo la Lindi wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.


Kitengo cha Mawasiliano