Habari

Imewekwa: Jul, 28 2021

​Serikali kumaliza uhaba wa majisafi Ruangwa

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema Wizara ya Maji imedhamiria na kujipanga kwa kuwatumia wataalam wake kumaliza uhaba wa huduma ya majisafi kwa wananchi wa Ruangwa.

Bofya HAPA kusikiliza Video

Mhe. Aweso amesema hayo akiwa katika mji wa Nandagala, Ruangwa akiwa amejumuika katika ziara ya kikazi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).

Waziri Aweso amesisitiza jukumu kubwa la viongozi ni kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo amewahakikishia wakazi wa Ruangwa kuwa kazi itakayofanyika ni kutumia chanzo kikubwa cha maji cha Mbwinji, kilichopo Ndanda ili kuwafikishia huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa sababu wataalamu wamebaini vyanzo vya maji vilivyopo Ruangwa sio toshelevu na vina madini mengi ya chumvi.