Habari

Imewekwa: Sep, 19 2023

Serikali kufikisha maji katika kata mbili zilizobaki Kilwa.

News Images

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishiwa wananchi wa kata za Limaliyao na Kivinje jimbo la Kilwa Kusini kuwa serikali inaendelea na jitihada kuhakikisha huduma ya majisafi, salama nayenye kutosheleza inafikishwa katika kata hizo.

Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko mara baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Ally Kasinge ambaye amesema kata hizo bado hazijafikiwa na huduma ya majisafi.

"Mhe. Mbunge maendeleo ni safari. Tumeshaianza safari kwenye kata nyingine,lengo letu ni kuhakikisha hizo kata mbili zilizobaki pia zinafikiwa na huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza"

Rais Samia amesema na kusisitiza kuwa ahadi ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza inamfikia kila Mwananchi.

Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini ambapo Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameshiriki katika ziara hiyo katika kuhakikisha maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na Rais yanatekelezwa kwa wakati na viwango.

Kitengo cha Mawasiliano