Habari

Imewekwa: Sep, 18 2023

​Ruangwa washukuru kwa miradi ya maji

News Images

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha nyingi ambazo zimewezesha utekekezaji wa miradi ya Maji.

Mhe. Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa ametoa pongezi hizo kwa Mhe. Rais Samia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Maonesho Kilimahewa, Ruangwa mjini.

Amesema kupitia Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) zaidi ya shilingi bilioni 184 zilitolewa na kuwezesha utekelezaji wa mradi ambao umehudumia mji mdogo wa Nyangao hadi Ruangwa na hivyo kuwezesha zaidi ya vijiji 55 kupata huduma ya maji.

Amesema Wizara ya Maji imetekekeza miradi mingi na inaendelea na utekekezaji ambao unatoa matumaini kwa wananchi wa Ruangwa.

Ameishukuru Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri wa fedha kwani miradi iliyotekekezwa inathibitisha viwango na ubora unaostahili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kikazi mikoa ya kusini ambapo Tarehe 17 Septemba ameanza ziara katika mkoa wa Lindi.

Kitengo cha Mawasiliano