Habari

Imewekwa: May, 27 2024

​Mradi wa Maji wa Same – Mwanga wafikia asilimia 90, Waziri Aweso awasha pampu kusukuma maji

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewasha pampu ili kusukuma maji kwenda katika tanki la Kivengere ambapo ujenzi wa mradi huo umefika asilimia 90 ya utekelezaji.

Waziri Aweso amekagua mradi huo mwanzo hadi mwisho na kuona utekelezaji wake kwa kushudia kukamilika kwa mifumo ya kutibu maji na kisha akafanya zoezi la kuwasha pumpu za kusukuma maji kupeleka kwenye tanki la maji la Kiverenge.

Katika ukaguzi huo, amefika eneo la Lembeni nakuona shughuli ya kupitisha bomba kuvuka chini ya barabara kubwa inayoelekea Moshi na kuelekeza kazi hiyo ikamilike ndani ya masaa 24 ili wananchi wapate huduma ya maji.

Ukaguzi uliofanywa na Waziri Aweso ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Makamu wa Rais Mhe Dkt. Philip Mpango katika kuhakikisha mwisho wa mwezi Juni 2024wananchi wa Same - Mwanga wanapata huduma ya uhakika ya majisafi na salama.

Waziri Aweso ameshuhudia mazingira magumu ya kazi katika kumaliza ujenzi wa mradi na ameridhishwa na morali pamoja na kasi iliyipo katika kufanikisha kazi hiyo na amewahakikishia wananchi wa Same-Mwanga-Korogwe kazi hiyo itakamilika kwa wakati kama maelekezo yalivyotolewa kuhusu kukamilisha mradi huo.

Kitengo cha Mawasiliano