Habari
Mhandisi Sanga akabidhi ofisi

Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga ambaye awali alihudumu katika nafasi hiyo katika Wizara ya Maji mapema leo amekabidhi ofisi na kuwataka watendaji na watumishi wote wa Sekta ya Maji kufanya kazi kwa juhudi na kusimamia mipango kuhusu huduma ya maji hapa nchini.
Amesema hayo leo Februari 28 wakati akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Maji, watumishi pamoja na watendaji wa taasisi za wizara kupitia mtandao wa video (video conference).
Mhandisi Sanga katika kikao hicho amesema kuwa na mpango kuhusu huduma ya maji ni jambo bora katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa huduma hiyo, hata inapotokea changamoto yoyote ya tabianchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amemshukuru Mhandisi Sanga kwa kuwajenga wataalamu wa Sekta ya Maji na kufanya kazi kwa umoja katika kufanikisha lengo la Serikali la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja katika kikao hicho amesema kazi inaendelea katika kufanikisha kazi zote ambazo zinaendelea katika sekta ya maji zinakamilika. Amewataka wadau wote wa sekta ya maji kushirikianavili kuhakikisha huduma ya maji inamfikia kila Mtanzania
Kitengo cha Mawasiliano