Habari
Dira za Maji za malipo kabla zaleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato

Matumizi ya Dira za maji za malipo kabla (Prepaid water meters) yameinua kiasi cha ukusanyaji wa mapato katika mradi wa maji wa Gidas wilayani Babati kutoka shilingi milioni 32 hadi milioni 500 kwa mwezi.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Babati mkoani Manyara Mhandisi Felix Molel katika amesema katika taarifa yake aliyoiwasilisha kwa
wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya RUWASA wakati wa ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala na Kamati ya Ukaguzi na Viashiria Hatarishi waliotembelea mradi huo kwa ili kutazama ufanisi wa Dira za malipo kabla.
Amesema Dira hizo zimeongeza uwazi katika makusanyo kutokana na matumizi ya mifumo inayowawezesha wananchi kutumia kadi maalum kuchota maji wakati wowote wanapohitaji huduma.
Kamati hizo zikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala Prof. Aloys Mvuma zimeambatana na wataalam mbalimbali wa RUWASA pamoja na wataalam wa Chuo cha Ufundi Arusha ambao ndiyo wabunifu na watengenezaji wa Dira hizo.